Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Selemani Jafo ametangaza kuongeza siku tatu za uandikishaji kwenye Orodha ya Wapiga Kura, uandikishaji sasa utakamilika Alhamisi Oktoba 17, 2019.
Wakati huo huo, zaodo ya watu Milioni 11 wameshajiandikisha katika daftari la kupiga kura nchi nzima hadi kufikia jana huku lengo likiwa ni watu zaidi ya milioni 26 kujiandikisha katika daftari hilo.
Akizungumza mara baada ya kutembelea vituo vya kujiandikisha katika daftari la kupiga kura mkoani Morogoro, Waziri Jaffo amesema uhamasishaji zaidi unahitajika kwa wananchi kupata elimu ya umuhimu wa kujiandikisha ili waweze kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji unaotarajia kufanyika Novemba 24 mwaka huu nchi nzima.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.