ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 13, 2019

WAZIRI KIGWANGALLA KUONGOZA WASHIRIKI MBIO ZA ROCK CITY MARATHON

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla anatarajiwa kuongoza maelfu ya washiriki wa mbio za Rock City Marathon zinazoratarajiwa kufanyika Octoba 20, mwaka huu kwenye viunga vya Jengo la Biashara la Rock City Mall, jijini Mwanza.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa mapema hii leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya mbio hizo, Bw Clement Mshana, ushiriki wa Waziri Kigwangalla unaenda sambamba na ushiriki wa viongozi wengine waandamizi wa serikali kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Bw John Mongella ambaye tayari amethibitisha kushiriki katika mbio za KM 42.

“Uwepo wa Waziri mwenye dhamana na masuala ya utalii kwenye mbio hizi unatokana na yeye kuunga mkono agenda iliyobebwa na mbio hizi ambayo mbali na kukuza vipaji vya mchezo huo ni kutangaza utalii hususani katika ukanda wa Ziwa kupitia mchezo wa riadha,’’ alisema

“Ukanda wa Ziwa una vivutio vingi ambavyo lazima vitangazwe kimataifa kwa nguvu kubwa zaidi na mbio hizi zimekuwa kama chachu ya kufanikisha agenda hiyo hususani kwa mwaka huu ambapo zinatarajiwa kuhusisha wadau wengi zaidi wa masuala ya utalii ambao pamoja na mambo mengine watapata fursa ya kuonesha bidhaa na huduma zao kwenye viunga vya mbio hizo’’ alibainisha.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.