ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 13, 2019

Mtoto mwenye umri wa siku mbili akutwa Jalalani


Mtoto mchanga amekutwa ametupwa jalalani katika kitongoji cha Majengo wilayani Manyoni mkoani Singida.

Inaelezwa kuwa mwili wa mtoto huyo ambaye anakadiriwa na umri wa siku mbili umekutwa umetupwa katika eneo la kukusanyia taka huku mzazi wa mtoto huyo akiwa bado hajajulikana.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Manyoni, Dokta. Furaha Mwakafwila Akithibitisha kupokea mwili wa mtoto huyo amesema wamepokea mtoto huyo akiwa ameshafariki ambapo amebainisha kuwa kuwa huenda mtoto huyo amefariki ndani ya masaa 24 mpaka muda waliompokea.

Diwani wa kata ya Manyoni mjini, Maghembe Machibula na Mwenyekiti wa kitongoji cha Majengo, Silvester Msogoti wamewataka wakazi wa kitongoji hicho kushirikiana na Jeshi la Polisi katika kutoa taarifa za mtu yeyote aliyehusika kumtupa mtoto huyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.