Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa anakagua barabara ya kutoka Mtili hadi Mpangatazara
Kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Injinia Selemani Mjohi akielezea jinsi ambazo watatengeneza barabara ya Mtili hadi Mpangatazara
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini Mahmoud Mgimwa akimuonyesha Kaimu meneja wa TARURA wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Injinia Selemani Mjohi ubovu wa daraja la Nandala
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Mbunge wa jimbo la Mufindi kaskazini
kutatua changamoto ya barabara kwa wananchi wa tarafa ya Ifwagi kuanzia mwezi
wa kumi mwaka huu kwa kuwa changamoto hiyo imekuwa ikirudisha nyuma maendeleo
kwa wananchi wa tarafa hiyo.
Akizungumza kwenye mikutano ya
hadhara ya kata za Mpangatazara,Ihanu na Ifwagi mbunge Mahmoud Mgimwa alisema
kuwa changamoto ya barabara imekuwa kero kwa kurudisha nyuma juhudi za
maendeleo ya wananchi wa tarafa ya Iwagi.
“Kweli hata mimi nimekuwa
nikiiona changamoto hii na imekuwa inaninyima usingizi mara kwa mara kwa kuwa
inakwamisha maendeleo ya wananchi kwa kuwa shughuli nyingi za kimaendelo
zimekuwa zinategemea barabara kwa kiasi kikubwa” alisema Mgimwa
Mgimwa alisema kuwa wamepata
kiasia cha shilingi milioni mia tisa ishirini na moja kwa ajili ya kutengeneza
barabara ya kutoka Mtili,Ifwagi,Lulanda hadi Mpangatazara kwa kiwango cha
changarawe ili kutatua tatizo hilo kwa muda mrefu.
“Jamani msione nilikuwa
sionekani wala siji kwenye mikutano ya hadhara kwa sasbabu barabara hii ilikuwa
inaniumiza kichwa ila kwa sasa nakuja kifua mbele na kiburi kwa kuwa tayari
fedha nimetafuta na nimewapa hawa TARURA kwa ajili ya kutengeneza barabara hii”
alisema Mgimwa
Mgimwa alisema kuwa barabara
hiyo itatengenezwa kwa kiwango bora ambacho kinaweza kudumu kwa miaka mitano
bili kuharibia kwa kiasi kikubwa bali kutakuwa na matengenezo madogo madogo
ambayo hayaepukiki.
Aidha Mgimwa amewataka wananchi
ambao wanapitiwa na barabara hiyo kuakikisha kuwa barabara hiyo inatengenezwa
kwa kiwango kulingana na gharama ambazo wamezitoa kwa kuwa fedha inayotumika
hapo ni kodi ya wananchi na wao ndio wenye mali hiyo.
“Barabara hii ikianza
kutengenezwa ni jukumu letu sote kuhakikisha inatengenezwa kulingana na michoro
iliyopo kwa mujibu wa mkataba la sivyo wasiipokee barabara hiyo
ikikamili,mkipokea barabara ambayo ipo chini ya kiwango hilo litakuwa sio
jukumu langu kwa kuwa wajibu wa kutafuta fedha mimi kama mbunge nimeshalifanya”
alisema Mgimwa
Kwa upande wake kaimu meneja wa
TARURA wilaya ya Mufindi mkoani Iringa Injinia Selemani Mjohi alikiri kwenye
mikutano ya hadhara kupokea fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara hiyo kwa
kiwango cha changarawe.
“Ni kweli mbunge wenu ametafuta
fedha kwa ajili ya kutengeneza barabara hii milioni mia tisa ishirini na moja
na tayari zipo benk kwenye akaunti zetu na tunarajia kuanza kuzitumia hivi
karibu kwa lengo la kutatua changamoto hii ambao imekuwa kero kwenu” alisema
Mjohi
Mjohi aliongeza kuwa tayari
walishatangaza zabuni na wameshawapata wakandarasi wawili ambao watahusika
kutengeneza barabara hiyo kwa kuwagawana kimeta ambazo zipo kwenye barabara
hiyo.
“Niwatoe hofu kuwa wakandarasi
wataanza kazi mapema mwezi wa kumi mwaka huu kutengeneza barabara yetu kwa kuwa
mwezi huu watasaini mikataba ya kuanza kazi na watapita kila kijiji kutoa
taarifa kuwa wanaanza kazi ya ujenzi wa barabara hizo” alisema Mjohi
Mjohi aliungana na mbunge wa
jimbo hilo Mahmoud Mgimwa kwa kuwataka wananchi kusimamia utengenezwaji wa
barabara hiyo kulingana na michoro watakayo pelekewa ili kuhakikisha ubora wa
kutengeza barabara hiyo unazingatiwa na ni jukumu lao.
“Nao baadhi ya wananchi
walimpongeza mbunge huyo kwa juhudi anazozifanya kuhakikisha analeta maendeleo
kwenye jimbo hilo na kusema kuwa wanamshukuru endapo barabara hizo zitakamilika
kutengenezwa” walisema wananchi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.