Erasto Ching'oro ambaye ni msemaji wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Idara Kuu Ya Maendeleo ya Jamii amesema kuanzia KESHO Alhamisi Agosti 8, 2019 unaanza usajili wa taasisi zilizosajiliwa kama kampuni lakini zinatekeleza majukumu ya taasisi zisizo za kiserikali (NGO).
Amesema usajili huo umegawanywa katika kanda tano ili kurahisisha mchakato huo.
Ching'oro ametoa kauli mapema hii leo katika mkutano na wandishi wa Habari kwa ajili ya kutoa taarifa ambayo imenuiwa kuwafikia wadau husika wa maeneo ya Kanda ya Ziwa.
Katika Bunge la bajeti lililomalizia Juni 28, 2019 ulipitishwa muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali wa mwaka 2019 uliokuwa na marekebisho ya sheria nane, zikiwemo Sheria ya Mashirika yasiyo ya Kiserikali (sura ya 56) na Sheria ya Makampuni (sura ya 212).
Muswada huo ambao umeshapitishwa bungeni miezi miwili iliyopita inazitaka kila asasi za kujisajili upya badala ya awali kusajiliwa na taasisi nyingine ikiwemo Wakala wa Usajili wa Leseni na Biashara (Brela).
Msemaji huyo wa Wizara ya Afya amefunguka zaidi kwa kusema kuwa fomu za maombi ya usajili huo zitapatikana katika ukumbi maalum ulioteuliwa katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Mwanza nao wadau wa BRELA kuwepo tayari na endapo muombaji akikamilisha taratibu zake kwa ufanisi ndani ya siku 14 atakabidhiwa cheti chake cha usajili ili atekeleze majukumu yake kwa ufanisi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.