ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 7, 2019

WAZIRI MKUU AONGOZA UJUMBE WA SERIKALI YA TANZANIA MAZISHI YA MKE WA MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI

HATIMAYE Mwili wa Natalia Bahati Kilangi ambaye alikuwa mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Professa Adelardus Kilangi umezikwa leo majira ya saa nane mchana nyumbani kwake, Luchelele, wilayani Nyamagama mkoani Mwanza.

 Viongozi mbalimbali wamejitokeza leo Jumatano Agosti 7,2019 katika ibada hiyo inayoongozwa na Makamu wa Rais wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Askofu Flavian Kasala.

Akiongoza ujumbe wa Serikali Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasihi viongozi wa dini na wadau mbalimbali kumuombea Professa Kilangi na familia yake kwa kuwa wanapitia katika kipindi hiki kigumu hasa ikizingatiwa kuwa mkewe ndiye aliyekuwa tulizo kwa Profesa Kilangi ambaye amekuwa mshauri mkubwa wa Serikali katika harakati mbalimbali za  Maendeleo. 

Baadhi ya viongozi wa kisiasa na kiserikali waliohudhuria ibada hiyo ni; Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, Msajili wa vyama vya siasa, Jaji Francis Mtungi na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally.

Natalia ambaye ni mke wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Professa Adelardus Kilangi alifariki Jumamosi iliyopita ya Agosti 3, 2019 saa 7 mchana katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza alipokuwa akiendelea na matibabu ya ugonjwa wa kiharusi.

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk Bashiru Ally akitoa heshimaza mwisho mbele ya mwili wa marehemu Natalia Bahati Kilangi katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marejemu kata ya Luchelele wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Natalia Bahati Kilangi katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marejemu kata ya Luchelele wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
 Mkuu wa Wilaya yaNyamagana Dkt Philis Nyimbi akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Natalia Bahati Kilangi katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marejemu kata ya Luchelele wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
 Akiwa ameambatana na bintiye Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania, Professa Adelardus Kilangi akitoa heshima za mwisho mbele ya mwili wa marehemu Natalia Bahati Kilangi katika ibada ya mazishi iliyofanyika nyumbani kwa marejemu kata ya Luchelele wilayani Nyamagana mkoani Mwanza.
Pia anayefuata nyuma (kijana mdogo) ni mtoto wa marehemu...Ni huzuni tupu imetawala hapa.
Pole rafiki.
 Mtoto wa kwanza wa marehemu.
Ibada ya mazishi inaendelea.
Safu ya watumishi wa Mungu.


1 THE. 5:18 SUV


Shukuruni kwa kila jambo; maana hayo ni mapenzi ya Mungu kwenu katika Kristo Yesu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.