Klabu ya waandishi wa habari ya Mkoa wa Mwanza(MPC)
imepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha waandishi wa habari wa Azam Media, kilichotokea leo tarehe 08/07/2019 katikati ya Mkoa wa Tabora na Singida.
Mwenyezi Mungu awape pumziko la milele
Pia tuungane sote kwenye maombi kuwaombea majeruhi walionusulika kwenye ajali hiyo Mungu awaponye kwa haraka ili warejee na kuendelea na majukunu yao ya kazi.
Klabu yetu (MPC) inawapa pole ndugu wote wa marehemu, Azam Media, waandishi wa habari na watanzania kwa msiba huu mkubwa kwa Taifa letu...Bwana alitoa na Bwana alitwaa jina la Bwana lihimidiwe Amina.
Tunaamini sisi tuliwapenda lakini Mwenyezi Mungu amewapenda zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.