ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, June 17, 2019

TANZANIA KUSHIRIKI MKUTANO WA KIDUNIA WA TEITI.


Mkutano wa 8 wa Kidunia   wa Uwazi na Uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimari za Nchi (TEITI), unataraji kuanza kesho hapa mjini Paris Nchini ufaransa.

Tanzania ni miongoni mwa Nchi zitakazoshiriki mkutano  huo ili kujadili kwa pamoja mafanikio ya mkakati wa uwazi na uwajibikaji katika usimamizi wa rasilimari za Nchi.

Timu ya washiriki wa mkutano huu toka Tanzania tayari imekwishawasili jijini Ufaransa ili kushiriki mkutano huo.

Washiriki wa Tanzania katika mkutano huo wametoka katika sekta mbalimbali, wapo waliotoka serikalini, kamati ya TEITI, Asasi za kiraia  na Waandishi wa Habari.

Kwa upande  wa Serikali Waziri wa Madini, Doto Biteko ameongoza msafara kwenye ushiriki wa  mkutano huo, ambapo leo siku moja kabla ya kuanza kwa  mkutano rasmi  hapo kesho  anashiriki mkutano mdogo(side event) unaojadili nafasi ya wachimbaji wadogo katika maendeleo ya sekta ya madini na matumizi ya takwimu kwenye madini.

Pia kwa upande wa kamati ya TEITA Tanzania, Mwenyekiti wa kamati hiyo Bwana Utour Ludovick na baadhi ya wajumbe wamewasili tayari kwa kuhudhuria mkutano huo.

Kwa upande wa baadhi  asasi za kiraia zilizopata nafasi ya kuhudhuria ni Haki Rasilimali ikiongozwa  na Mratibu wake Bi Recho Changonja na pia asasi ya kukuza utawala bora na uwazi Tanzania.

Pia katika kuhakikisha washiriki toka asasi za kiraia wanashiriki, shirika la kimataifa la Hivos Afrika ya mashariki linalohimiza uwazi katika mikataba (Open Contracting) na kuwajengea uwezo waandishi wa habari limewawezesha washiriki toka asasi za kiraia  na waandishi wa habari kushiriki mkutano huo ili kupata ufahamu mzuri wa namna ya kuhimiza uwazi na uwajibikaji katika rasilimali za Nchi.

Mkutano huo utakuwa ni wa siku mbili kuanzia Julai 18 - 19 utakaofanyika katika ukumbi wa OECD katikati ya Jiji la Parisi na ufanyika kila baada ya miaka mitatu ambapo Nchi washiriki wa mpango wa TEITI ukusanyika na kupata nafasi ya kujadili, mafanikio, changamoto na kutoka na maazimio.

Na.
 Edwin Soko 
 Gsengo TV
 Paris Ufaransa

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.