Taarifa kwa vyombo vya habari
Tamko la asasi za kiraia Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika kwenye utekelezaji wa mkakati wa uwazi na uwajibikaji kwenye usimamizi wa rasilimali za Nchi
Katika mkutano wa Kidunia wa 8 wa uwazi na uwajibikaji ulioanza Juni 17- 19 , 2019 Jijini Paris Asasi za kiraia za Afrika zimetoa mapendekezo yafuatayo ili kuhimiza suala la uwazi na uwajibikaji kwenye kulinda rasilimali za Nchi.
...............................
1.katika utekelezaji wa mkakati wa uwazi wa rasimali kwa Nchi za Msumbiji, Uganda, Tanzania na Zambia miongozo mipya ya uwazi kwenye usimamizi wa rasilimali isaidie kuboresha taarifa zilizopo kwenye masuala ya uwazi ili kuleta ufanisi wa utekelezaji wa mkakati wa huo na kuleta tija Afrika.
2.Kwa Nchi za Kenya na Zimbambwe tayari zimeonyesha nia ya kujiunga kwenye mpango wa uwazi na uwajibikaji wa kulinda rasilimali za Nchi(EITI) sheria za kimataifa zenye miongozo ya utekelezaji wa mkakati wa EITI ziwe ni fursa kwa asasi za kiraia na vyombo vya habari kuhimiza uwazi kwenye rasilimari za Nchi zao kwani zitawapa ushiriki mpana wa kufuatilia utekelezwaji wa uwazi kwenye maeneo ya rasilimari za Nchi.
3. Kwa nyiongeza wadau kama Asasi za kiraia na vyombo vya habari katika ukanda wa Afrika watakuwa wamepiga hatua moja mbele kwenye kupata taarifa na takwimu kutokana na kuwepo kwa mkakati wa uwazi katika usimamizi wa rasilimari tofauti na awali hivyo ni wajibu wao kuhimiza kuboreshwa na kutungwa kwa sheria mpya na kubadilishwa kwa sera zilizopo ili kupata sheria na sera nzuri kwa lengo la kuongeza uwazi ambazo zitasaidia kwenye maeneo yafuatayo.
a. kuripoti juu ya mazingira.
Viwango vya mpango wa uwazi na uwajibikaji kwenye rasilimali sio tu vihimiza makampuni ya uchimbaji wa rasilimali yaripoti juu ya athari za kimazingira kwenye miradi ya uchimbaji bali yaende mbali kwenye kuweka wazi suala la mazingira na mizania ya malipo wanayolipa kwenye sekta ya madini.
b.Uwakilishi na ushiriki
wa nafasi ya wanawake katika sekta ya rasilimali uendane sawa kama ulivyo ushiriki wa wanaume. Suala la jinsia lipewe msisitizo na kuondoa ombwe lililopo kwenye sekta ya rasilimali za Nchi kati mwanaume na mwanamke.
c. Fungate na ushirikiano
Kuanzishwa kwa mkakati wa uwazi kwenye usimamizi wa rasilimali (EITI) kulenge kuhamasisha uwazi na uwajibikaji miongoni mwa Nchi tajiri kwenye kusimamia miongozo mbalimbali kama muongozo wa Umoja wa Ulaya na Canada. ESTIMA ili ulete mabadiliko na kututoa kwenye usiri tuliouzoea.
Tamko hili limeandaliwa na asasi za kiraia zinazofanya ulaghibishi kwenye maeneo ya rasilimali toka Tanzania, Zambia , Kenya, Uganda na Msumbiji.
Na kutolewa na
Recho Chagonja
17:06:2019
Paris
Imeripotiwa Na
Edwin Soko
Gsengo TV
Paris
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.