JAMHURI YA MUUNGANO
WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA
NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI (M) MWANZA
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
11.06.2019.
Tukio
la Kwanza
JESHI LA POLISI MKOA
WA MWANZA LINAMSHIKILIA KIJANA MMOJA AITWAYE MICHAEL MAYALA, MIAKA 16, MKAZI WA KISHINDA KWA TUHUMA ZA KUMBAKA BERTHA JOSEPH, MIAKA 13, MWANAFUNZI
WA DARASA LA NNE HUKU AKIWA AMEMZIBA MDOMO NA PUA KWA KANGA HADI KUPELEKEA KUPOTEZA MAISHA, KITENDO AMBACHO NI KINYUME
NA SHERIA
TUKIO HILO LIMETOKEA
TAREHE 05.06.2016 HUKO KATIKA KIJIJI CHA KISHINDA, WILAYA YA SENGEREMA, HII NI
BAADA YA MTUHUMIWA HUYO AKIWA NA BINAMU YAKE (MAREHEMU) NA NDUGU ZAO WENGINE WAWILI WANAOISHI WOTE HAPO
KIJIJINI KWA BIBI YAO WALIKWENDA SHAMBANI KUPALILIA MATUTA AMBAPO KILA MMOJA
ALITAKIWA KUPALILIA MATUTA MATANO(5).
AIDHA, WENZAO WAWILI
WALIMALIZA NA KUTANGULIA NYUMBANI WAKABAKI MTUHUMIWA NA MAREHEMU WAKIMALIZIA
KAZI NDIPO MTUHUMIWA ALIMKAMATA MAREHEMU NA KUMZIBA MDOMO NA PUA KWA KUTUMIA
KANGA ALIYOKUWA AMEVAA MAREHEMU KISHA KUMBAKA NA KUPELEKEA MAREHEMU KUPOTEZA
MAISHA PAPO HAPO.
BAADA YA TUKIO HILO
MTUHUMIWA ALIRUDI NYUMBANI NA ALIPOULIZWA NA WAZAZI KUWA MWENZAKE YUKO WAPI
ALIJIBU KATANGULIA KURUDI NYUMBANI, NDUGU WALIANZA KUMTAFUTA MAREHEMU BILA
MAFANIKIO NDIPO MTUHUMIWA ALITOROKA NYUMBANI KWENDA KIJIJI CHA KATUNGURU KWA
NDUGU ZAO WENGINE, FAMILIA ILIMTILIA MASHAKA NA BADAE WALIMKAMATA NA KUMPELEKA
POLISI ALIPOHOJIWA ALIKUBALI KUHUSIKA NA TUKIO HILO NA KUWAPELEKA POLISI HADI
SHAMBANI ENEO MWILI WA MAREHEMU ULIPOKUWA.
JESHI LA POLISI MKOA
WA MWANZA LINAENDELEA NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA
ATAFIKISHWA MAHAMANI. MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA
KUKABIDHIWA KWA NDUGU KWA AJILI YA MAZISHI.
Tukio
la Pili;
JESHI LA POLISI MKOA WA
MWANZA LINAMSHIKILIA JOHN SAMWELI, MIAKA
18, MKURYA, MKAZI WA IBANDA, KWA TUHUMA ZA KUMLAWITI MTOTO WA KIUME JINA TUNALIHIFADHI, MWENYE UMRI WA MIAKA
MIWILI NA NUSU NA KUMSABABISHIA MAUMIVU MAKALI SEHEMU ZA SIRI, KITENDO AMBACHO
NI KOSA LA JINAI.
TUKIO HILO LIMETOKEA
TAREHE 10.06.2019 MAJIRA YA SAA 13:00HRS HUKO MAENEO YA IBANDA KATA YA KIRUMBA
WILAYA YA ILEMELA, HII NI BAADA YA MTUHUMIWA KUMCHUKUA MTOTO NA KUMRUBUNI KUWA
ANAKWENDA KUMNUNULIA SODA NDIPO WALIPOFIKA VICHAKANI ALIBADILIKA NA KUMTENDEA
KITENDO HICHO CHA KIKATILI.
HATA HIVYO, WAKATI
MTUHUMIWA ANAENDELEA KUTENDA UNYAMA HUO. MTOTO ALIKUA AKIPIGA KELELE AKIOMBA MSAADA,
WATU WALISIKIA NA KWENDA KUMSAIDIA NDIPO WALIMKUTA MTUHUMIWA AKIWA ANAMLAWITI
MTOTO. WANANCHI WALITOA TAARIFA POLISI NDIPO ASKARI WALIFIKA KWA HARAKA ENEO LA
TUKIO NA KUFANIKIWA KUMKAMATA MTUHUMIWA.
JESHI LA POLISI
LINAENDELEA NA MAHOJIANO NA MTUHUMIWA PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ATAFIKISHWA
MAHAKAMANI. MTOTO AMEPELEKWA HOSPITALI YA MKOA SEKOU TOURE KUPATIWA MATIBABU NA
HALI YAKE INAENDELEA VIZURI.
JESHI LA POLISI MKOA
WA MWANZA LINATOA ONYO KWA BAADHI YA VIJANA WENYE TABIA CHAFU NA YA KIKATILI YA
KUBAKA/KULAWITI KUWA WAACHE KWANI NI KINYUME NA SHERIA NA ENDAPO MTU/WATU
WATABAINIKA HATUA KALI ZA KISHERIA ZITACHUKULIWA DHIDI YAO.
IMETOLEWA
NA;
MULIRO
J MULIRO-ACP
KAMANDA
WA POLISI (M) MWANZA
11 JUNE, 2019.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.