Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu
Humfrey Polepole akitoa semina kwa makatibu wa idara ya Itikadi na uenezi wa mkoa wa Iringa iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
Mjumbe wa
halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa (MNEC) Salim Asas akiwahutubia makatibu wa idara ya Itikadi na uenezi wa mkoa wa Iringa walikuwa wakipewa semina na Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu
Humfrey Polepole juu ya Idara hiyo,semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo
Baadhi ya makatibu wa Idara ya Itikadi,siasa na uenezi mkoa wa Iringa wakiwa makini kumsikiza Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu
Humfrey Polepole alipokuwa anawafunda.
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Katibu wa itikadi,siasa na uenezi wa CCM taifa Ndugu
Humfrey Polepole Amewataka viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia chama hicho
kutokuwa chanzo cha migogoro na majungu bali wawe suluhisho kwa kuwa lengo la
chama ni kusimamia serikali na kuwaletea watanzania Maendeleo.
ameyasema hayo kwenye semina ya
kuwafunda katibu wa Idtikadi na uenzi wa ngazi zote mkoani Iringa, Polepole amesema
kuwa kuna baadhi ya viongozi wamekuwa chanzo cha migogoro hata kufanya
kurudisha nyuma maendeleo ya chama.
Amesema kuwa chama hicho kimejengwa
kwenye misingi bora kwa lengo la kutumikia wananchi na kusikiliza watu pamoja
na kujua shida zao lakini kuna baadhi yao wanaleta majungu wao kwa wao jambo
linalofanya kutowavumilia.
“Sasa hivi hii ni ccm mpya
chini ya mwenyekiti Dr John Pombe Magufuli na hana utani anataka kazi tu na
wale ambao wanaona wameshindwa watupishe maana unapoacha sumu ndani si ya siku
itakudhuru tunapogombana wanaoumia ni watanzania waliotupa dhamana ya kusimamia
serikali”Alisema Polepole
Polepole ameongeza kuwa kwasasa
mlango uko wazi endapo mtu anaona atashindwa kupelekana na kasi ya CCM mpya
chini ya mwenyekiti wao John Pombe Magufuli ni vyema akapisha na kuacha
wanaojua kufanya kazi.
Hata hivyo Polepole amewataka
viongozi kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa huku akimtaka katibu wa itikadi na
uenezi mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza kuunganishi vizuri na kuendelea kuwatumikia
wananchi vizuri kwa kueleza mambo mazuri yanayofanywa na serikalia ya CCM.
Vile vile Polepole amewasifu
viongozi katika ngazi zote kwasababu wameibadilisha ccm na wananchi wameelewa
dhamira ya Chama katika kuisimamia serikali.
Aidha Polepole alisema kuwa chama cha
mapinduzi kikifanya vibaya kwa wananchi ujue kuwa idara ya Itikadi na uenezi
haijafanya kazi yake ipasavyo,hivyo ni lazima kila kiongozi awajibike ipasavyo
ili kutimiza malengo ya chama.
“Tunatakiwa kushughulikia
matatizo ya wananchi kwa kuwapa mafunzo mbalimbali viongozi wa ngazi za chini
ili kueneza vilivyo cha hicho ambacho kipo madarakani muda mrefu sasa” alisema Polepole
Polepole aliwaambia viongozi
hao kuwa uongozi ni kujitolea na sio kutegemea kupata maslai furani kwenye
chama wakati unagombea nafasi mbalimbali lazima uwe unasehemu ya kuingiza
kipato kingine na usitegemee kuvuna kutoka kwenye chama.
Kwa upande wake mjumbe wa
halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi Taifa (MNEC) Salim Asas
alimtaka katibu wa itikadi na uenezi mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza kuratibu
namna nyingine tena ya kuwawezesha makatibu hao kuanzia ngazi ya chini hadi juu
kupata fedha za kufanyia kazi mafunzo walipata kutoka kwa katibu wa
itikadi na uenezi wa CCM taifa Ndugu Humfrey Polepole.
“Ramadhani Baraza nakuomba
uratibu zoezi hilo ili tuone jinsi ya kuwasaidia makatibu hao ili waweze
kukieneza vilivyo cha chetu kwa wananchi wote huko waliko” alisema Asas
Naye katibu wa itikadi na
uenezi mkoa wa Iringa Ramadhani Baraza alisema ameyapokea maagizo yote na
atayafanyia kazi ili idara hiyo mkoa wa Iringa iwe mfano kwa mikoa mingine hapa
nchini.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.