Timu ya vijana ya Yanga chini ya miaka 20 imewaduwaza vijana wenzao wa Simba kwa kuwachapa mabao 2-1 katika mchezo wa kundi A hatua ya nane bora ya ligi kuu Tanzania Bara kwa vijana inayoendelea kwenye Dimba la Azam Complex Chamazi, jijini Dar es Salaam. Simba ndiyo waliotangulia kupata bao dakika ya 27 kupitia kwa Jackson James, lakini Yanga walitumia dakika nne za mwisho kupata pointi tatu muhimu, wakianza kusawazisha dakika ya 90 kupitia kwa Yassin Salah, kabla ya Erick Msagati kupachika goli la ushindi dakika ya 90+4.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.