ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, June 15, 2019

MWANZA YAJADILI ONGEZEKO KUBWA LA WAMACHINGA LISILOENDANA NA IDADI YA WATEJA



Serikali imeshauriwa kutunga sera inayotambua wafanyabiashara wadogo al-maarufu MACHINGA ili waweze kutoa mchango wao katika kukuza pato la taifa.

Ushauri huo umetolewa na mhadhiri wa Chuo Cha Elimu ya Biashara - CBE DKT.NASIBU MRAMBA wakati akiwasilisha matokeo ya utafiti kuhusu mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara wadogo (MACHINGA) jijini mwanza.

Utafiti uliofanywa na taasisi ya maendeleo jumuishi (I4ID) pamoja na shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana la KIVULINI umebaini kuwepo kwa ongezeko kubwa la wafanyabiashara wadogo katika jiji la Mwanza lisiloendana na idadi ya wateja.

Mhadhiri wa chuo cha elimu ya biashara (CBE)DKT. NASIBU MRAMBA amewasilisha matokeo ya utafiti huo kwa madiwani pamoja na watendaji wa manispaa ya Ilemela jijini Mwanza. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.