Mbunge wa Geita (CCM), Joseph Kasheku maarufu Musukuma ameiomba Wizara ya Afya kueleza chakula ambacho watu wasio na vitambi wanatakiwa kula ili nao wawe na vitambi.
Ametoa kauli hiyo leo Jumatano Mei 29, 2019 bungeni jijini Dodoma wakati akiuliza swali la nyongeza kwa Wizara ya Afya na kuzua gumzo katika chombo hicho cha kutunga sheria huku Spika Job Ndugai akiwataka wabunge kuandika mlo wanaotaka kula ili mgahawa wa Bunge uelezwe.
Katika swali lake hilo la nyongeza, Musukuma ameeleza jinsi watu wenye vitambi wanavyotakiwa kupunguza kiwango cha kula, kuhoji kuwa wasio na vitambi pia wanakula vyakula vya aina hiyo lakini hawapati, kuomba ushauri ni chakula gani watu wasio na vitambi wanatakiwa kula ili nao wavipate.
Akijibu swali hilo kwa niaba ya Waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile, naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega amemtaka mbunge huyo kuonana na wataalam wa afya ili wamshauri chakula anachopaswa kula ili aweze kuongezeka mwili.
Swali hilo la Musukuma lilikuwa gumzo baada ya wabunge wengi kusimama na kuuliza maswali ya nyongeza kufuatia swali la msingi lililoulizwa na mbunge wa Viti Maalum (CCM), Khadija Nassiri Ali.
Khadija alihoji mikakati ya Serikali katika kupambana na magonjwa yasiyoambukiza na mbinu gani zitumike kupambana na kitambi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.