ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 20, 2019

RAIS FILIPE NYUSI: IDADI YA VIFO MSUMBIJI VINAWEZA KUFIKIA 1000

Rais Filipe Nyusi: Idadi ya vifo Msumbiji vinaweza kufikia 1000

Rais Filipe Nyusi wa Msumbiji amesema kuwa, kuna uwezekano idadi ya watu waliopoteza maisha kutokana na kimbunga cha Idai kilichoikumba nchi hiyo ya kusini mwa Afrika ikafikia watu 1000.
Rais huyo wa Msumbiji alisema hayo jana Jumatatu wakati alipozungumza na taifa kwa njia ya redio na kuongeza kuwa, maafa yaliyosababishwa na kimbunga hicho ni makubwa mno ikilinganishwa na idadi ya watu waliothibitishwa kufariki dunia hadi hivi sasa kutokana na maafa hayo ya kimaumbile.
Jana mashirika ya habari yalikuwa yametangaza kwamba, idadi ya watu waliothibitishwa kupoteza maisha kutokana na kimbunga cha Idai kilichopiga katikati ya Msumbiji wiki iliyopita imeshafikia 215. Kimbunga hicho kilichoziathiri pia nchi za Zimbabwe na Malawi kimesababisha mafuriko na uharibifu mkubwa.



Kwa mujibu wa vyombo hivyo vya habari, hadi jana Jumatatu watu wasiopungua 126 walikuwa wamethibitishwa kufariki dunia katika nchi mbili za Msumbiji na Malawi huku waziri wa habari wa Zimbabwe akisema hiyo jana kuwa watu 89 wamepoteza maisha nchini humo kutokana na maafa hayo ya kimaumbile.

Kwa mujibu wa televisheni ya al Jazeera ya Qatar, uharibifu wa janga hilo la kimaumbile ni mkubwa sana kiasi kwamba umefika umbali wa kilomita 300 kutoka eneo kilipopiga kimbunga cha Idai. Mamia ya nyumba zimeharibiwa kikamilifu katika mji wa Beira. Watu wengi wamekimbilia katika maeneo ya shule na wengine kwa majirani zao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.