ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, December 5, 2018

KIWANDA CHA WATENGENEZA FEDHA BANDIA CHANASWA JIJINI MWANZA.


GSENGO tV

Kuelekea sikuu za mwisho wa mwaka yaani Christmas na Mwaka mpya, Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza limetoa tahadhari kwa wananchi wake kujihadhari na kupokea au kumiliki fedha zisizo halali kwaajili ya malipo yaani fedha bandia.

Kauli hiyo imetolewa Leo na Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Jonathan Shanna mara baada ya kikosi chake cha upelelezi kuwanasa watu wa 5  maeneo tofauti tofauti Kiloleli wilayani ilemela mkoani Mwanza, Serengeti mkoani Mara na mwingine mkoani Kigoma ambao wote wanatajwa kuhusika na utengenezaji na umiliki wa karakana ya uchochoroni ya kutengeneza fedha bandia.....


Katika operesheni hiyo maalumu iliyochukua takbrani masaa 48 kuanzia tarehe 03/12/2018 majira ya 04/04/2018 imefanyika baada ya kupatikana kwa  taarifa za kiintelejensia kwamba katika mtaa wa Kiloleli B wapo watu wanaotengeneza noti bandia.


Baada ya kupatikana kwa taarifa hizo kikosi maalumu cha askari wa mikoa ya kanda ya ziwa toka Mkoa wa Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara na Tanapa – Serengeti kilifanya msako mkali katika mtaa huo na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa tajwa hapo juu wakiwa na kiasi hicho cha noti bandia.


Watuhumiwa wawili wamekamatwa maeneo ya Mugumu Serengeti ambao ni; Swedi Amani Mrete @ Kongo, miaka 40, mfanyabiashara, mkazi wa buhongwa Mwanza i Cosmas Busiga Bereka, miaka 40, fundi chuma, Mkazi wa Mandu Mwanza.

 Aidha watuhumiwa wengine wawili wamekamatwa mtaa wa Kiloleli B kwenye nyumba ambayo ndipo wanapotengenezea fedha hizo bandia ambao ni Baraka Dominiko Mwanga, miaka 26, mfanya biashara, mkazi wa kiloleli B, Khadija Musa Elias, miaka 20, mkulima, Mkazi wa Kiloleli B.

 Vilevile mtuhumiwa aliyetoroka amekamatwa huko mto Malagarasi Kasulu Kigoma, mtuhumiwa huyo ni v. Batisti Msafiri Katumbi, miaka 40, mfanya biashara, mkazi wa Igoma Mwanza Sambamba na hilo watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na noti hizo bandia zikiwa katika makundi yafuatayo;

 i. Noti za elfu kumi zimekamatwa zenye thamani ya kiasi cha laki mbili na elfu thelasini 
(TSH 2,230,000) 

 ii. noti za elfu tano zimekamatwa zenye thamani ya laki nne na elfu sabini (TSH 470,000/=)

 iii. Noti za elfu mbili zimekamatwa zenye thamani ya elfu sitini ( TSH 60,000/=). iv. Noti za dola mia kumi na nne. v Jumla kuu TSH 2,830,000/=

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.