ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 1, 2018

MAAMUZI YA SERIKALI KUONGEZA UZALISHAJI WA UMEME YAENDE SANJARI NA UTUNZAJI WA MAZINGIRA- DKT KALEMANI


NA AMIRI KILAGALILA/GSENGOtV

NJOMBE

Waziri wa Nishati DK.MEDARD KALEMANI amewataka Viongozi na wadau wa nishati kuwasaidia wananchi hususani wakazi wa mkoa wa Njombe kutunza vyanzo vya maji ili kuwezesha ukuzaji wa mto kilombero unaolisha maji yake mto Rufiji maalumu kwa mradi wa kuzalisha umeme wa rufiji wenye uwezo wa kuzalisha umeme takribani MW.2,1OO.

Waziri KALEMANI ameyasema hayo wakati wa mkutano wa uelewa wa mradi wa kuzalisha umeme wa rufiji (rufiji hydropower project) uliofanyika katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe ulio wakutanisha wadau mbali mbali wakiwemo wabunge na  viongozi wa halmashauri za mkoa wa Njombe.



Aidha dk.kalemani amesema kuwa serikali ya awamu ya tano imeamua kutekeleza mradi huo mkubwa wa mda mrefu ulionza kubuniwa tangu serikali ya awamu ya kwanza na leo umeanza kutekelezwa ukiwa na zaidi ya miaka 40 huku sababu kubwa ikiwa ni kuongezeka kwa matumizi makubwa ya umeme nchini.

Kalemani ameongeza kuwa licha ya hali ya umeme kwa sasa kuwa bora kwa kuwa na umeme wa ziada megawati 201 lakini haiwezi kutoshereza katika mahitaji ya uchumi wa viwanda ndio maana serikali imeamua kuongeza uzalishaji wa umeme mwingi na wakutosha  ambao ghalama yake ni naafuu licha ya serikali kuendelea kuzalisha umeme mchanganyiko ukiwemo wa gesi. 

Kwa upande wake kaimu mkuu wa mkoa wa Njombe ALLY KASINGE licha ya kupongeza jitihada za kuanza mradi huo mkubwa wa umeme nchini, amesema kuwa ikiwa Njombe ni miongoni mwa mikoa yenye vyanzo vingi vya maji yanayolisha mto rufiji wanayosababu ya kushiriki kikamilifu katika utunzaji wa vyanzo hivyo vya maji ili kusadia juhudi za wizara katika kufikia umeme wa kutosha kuelekea uchumi wa viwanda.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.