Picha ya mtandao
Watu wawili wamefariki na wengine wawili kujeruhiwa usiku wa kuamkia leo huko Dunga, Zanzibar, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kushika moto.
Taarifa kutoka eneo la tukio zinasema gari hilo aina ya Toyota IST lililokuwa likitokea Kiwengwa, lililipuka baada ya tenki lake la mafuta kuvuja kufuatia kugongwa na jiwe.
Majina ya waliofariki na kujeruhiwa yalikuwa hayajapatikana hadi tunakwenda mitamboni. Hata hivyo, tutawajuza wasomaji wetu mara tu tukipata habari zaidi kuhusu tukio hilo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.