Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye, akitoa taarifa ya Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa, wakati wa kufunga maadhimisho hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma jana.
Askari wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Kitengo cha Maokozi toka Makao Makuu wakimuonesha Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala, jinsi wanavyoweza kufanya maokozi kwenye majengo marefu pindi ajali inapotokea, alipotembela Uwanja wa Jamhuri Jijini Dodoma wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 Jijini humo jana.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Uhamiaji Dkt. Anna Makakala, akipokea zawadi ya kizimia moto cha awali (Fire Extinguisher) kutoka kwa Mkaguzi Msaidizi wa Zimamoto Philibert Chaki, alipotembelea banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 Jijini Dodoma jana.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye akimkabidhi cheti mwakilishi wa TCRA, ambaye jina lake halikupatikana kwa mchango wake wa kufanikisha Maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa, wakati wa kufunga maadhimisho hayo yaliyoanza Agosti 29, 2018 katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini Dodoma jana.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye akimkabidhi zawadi ya kikombe Konstebo wa Timu ya Polisi Dodoma, Ally Juma mara baada ya kufanikiwa kupata ushindi wa bao moja dhidi ya wapinzani wao Timu ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, mechi iliyochezwa katika Uwanja wa Jamhuri, wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 Jijini Dodoma jana.
Msanii Mrisho Mpoto na kundi lake
wakitumbuiza wimbo maalum wenye maudhui ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji, mbele
ya Mgeni rasmi Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamto na Uokoaji, CGF Thobias
Andengenye, wakati wa kufunga maadhimisho ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji
Kitaifa yaliyoanza Agosti 29, 2018 katika Uwanja wa Jamhuri uliopo Jijini
Dodoma jana. (Picha zote na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji)
Maadhimisho
ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa yalizinduliwa rasmi na Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Mhe. Kangi Lugola (Mb) Agosti 29, 2018 katika Uwanja cha
Jamhuri Jijini Doodma na kufungwa jana Agosti 31, 2018 na Kamishna Jenerali wa
Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, CGF Thobias Andengenye. Kauli mbiu ya Maadhimisho
ya Wiki ya Zimamoto na Uokoaji Kitaifa mwaka huu ni “SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA
KWA KUFUNGA VING’AMUAMOTO VIWANDANI”
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.