ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, September 5, 2018

KILIO CHA MAGUFULI KWA VIWANDA VYA BABA WA TAIFA.

 UKEREWE. Rais John Magufuli ametumia mkutano wake wa hadhara mjini Nansio Ukerewe kuelezea masononeko yake kuhusu kudorora, kufilisika na kufa kwa viwanda vingi vilivyojengwa wakati wa Serikali ya awamu ya kwanza iliyoongozwa na Mwalimu Julius Nyerere na kuwataka Watanzania kila mmoja kujiuliza Taifa lilijikwaa wapi.

"Kulikuwa na viwanda vya kuchambua pamba; na pamba ya Ukerewe ilikuwa bora katika soko la dunia. Lakini leo hakuna, vimekufa vyote. Hebu tujiulize tumejikwaa wapi na tutarekebishaje," amesema Rais Magufuli huku umati unaomsikiliza ukiwa kimya
Ametaja viwanda vingine vilivyokufa kuwa ni vya korosho, kahawa, zabibu na tumbaku kiwanda cha TANALEC Arusha ambavyo Watanzania wanapaswa kujiuliza vilikufaje?
Huku umati ukiwa umetulia kimya tofauti na awali ulipokuwa ukishangilia, Rais Magufuli ametaja mali na rasilimali nyingine za umma zilizokufa kutokana na usimamizi na matumizi mabaya kuwa ni pamoja na meli 14 ambazo tano pekee zinafanya kazi baada ya kukarabatiwa.







Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.