Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli (katikati) akizindua kiwanda cha Lakairo kilichopo eneo la Isangijo wilayani Magu Mkoani Mwanza. |
Rais John Pombe Magufuli ameagiza msamaha wa kodi unaotolewa kwa wawekezaji wa nje uanze kunufaisha wawekezaji wa ndani ili kutoa usawa wa ushindani kwenye soko.
Amesema si sawa kwa wawekezaji kutoka nje kupewa msamaha wa kodi hadi wanapoanzisha biashara lakini wale wa ndani ambao wengi ni wazawa wanatozwa kodi hata kabla ya kuanza uzalishaji.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania John Pombe Magufuli |
Akizungumza muda mfupi baada ya kuzindua kiwanda cha Lakairo kilichopo eneo la Isangijo wilayani Magu leo Septemba 4, 2018 Rais Magufuli ametoa mfano wa mwekezaji ambaye hakumtaja jina anayezalisha taulo za kike ambaye malighafi anayoagiza kutoka nje inatozwa kodi huku taulo za kike zinazoingizwa kutoka nje zikipata msamaha wa kodi.
Mbunge wa Magu (CCM), Boniventura Kiswaga ametumia fursa ya kusalimia wananchi na kumwomba Rais Magufuli kusaidia kumaliza tatizo la maji na miundombinu inayoikabili wilaya ya Magu.
Akijibu maombi hayo, Rais Magufuli ameagiza Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (Tarura), kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka njia kuu ya Mwanza-Musoma hadi kituo cha Utamaduni cha Bujora.
RAIS MAGUFULI AZINDUA KIWANDA CHA LAKAIRO INDUSTRIES GROUP LIMITED
AIGIZA WIZARA YA FEDHA NA VIWANDA KUIANGALIA UPYA TAXI HOLIDAY *Awashauri Wabunge wanaoweza kukopa wakope na kuanzisha viwanda vitakavyotoa ajira kwa WATANZANIA
*Ampongeza Mkurugenzi Mkuu wa Lakairo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amezindua KIWANDA cha LAKAIRO Industries Group Limited na kutoa agizo kwa Wizara ya fedha na wizara ya viwanda kuiangalia namna ya kuwasaidia na kuwawezesha wawekezaji wazalendo.
Hayo ameyasema LEO Sept 4, 2018 wakati akizungumza na wananchi pamoja na viongozi mbalimbali walifika kwenye uzinduzi wa KIWANDA hicho ambacho kinamilikiwa na mwekezaji mzalendo na mbunge wa Rorya Lameck Ailo.
Mbali na hilo Mhe. Rais ameitaka wizara ya fedha, viwanda na biashara kuliangalia upya suala la taxi hpliday ambayo hupewa wawekezaji wa nje ambayo hutumiwa vibaya na baadhi yao kwa kuchuma faida na badae wanakabidhi kwa mtu mwingine au kama KIWANDA anakiuza, huku akitolea mfano Jiji la Dar es salaam.
. “Nafahamu huwa mnatoa Taxi holiday kwa wawekezaji kutoka nje, mnawapa kipindi fulani wafanyekazi zao bila kulipa kodi mpaka watakapojijengea uhalali” alisema Mhe. Rais “na mara nyingi wawekezaji wa namna hiyo wakishakaa hiyo miaka mitano kama ni KIWANDA anakiuza, au anampa mwingine” aliongeza "Tumekuwa tukipigwa sana WATANZANIA kwa mchezo huo hivyo nawaomba wizara ya fedha na wizara ya viwanda kuangalia upya ili hawa wawekezaji wa ndani wafaidike na zaidi angalieni namna ya kuwasaidia. .
KIWANDA hicho kilichopo Isangijo wilayani Magu Mkoani Mwanza kimeajili vijana 400 kinatengeneza bidhaa za pipi, mifuko, still wire, Roll pop na jojo.✔
Mbunge wa Jimbo la Misungwi Mhe. Kitwanga al maarufu "Mawe Matatu' naye amekuwa mmoja kati ya wageni waliohudhuria hafla hiyo
Mhe. Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akihutubia kwenye hafla hiyo.
Mamia ya watanzania wamejitokeza hapa kushuhudia uzinduzi huo sanjari na kumsikiliza Mhe. Rais.
Jiwe la msingi.
Himaya ya Jiwe la Msingi.
Kiwanda tayari kwaajili ya kazi, kukuza uchumi na ajira.
Wafanyakazi, Wadau wa Biashara, Wananchi, Mabibi na Mabwana wote wamejitokeza hapa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.