RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa Vituo vya Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibar na Uzinduzi wa Uimarishaji Mfumo wa Usajili kielektroniki, (kushoto_ Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe. Haji Omar Kheri, na (kushoto) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi, wakishuhudia hafla hiyo iliofanyika katika viwanja vya Ofisi hiyo Dunga Wilaya ya Kati Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua jengo la Ofisi mpya za Wilaya -Dunga pamoja na uzinduzi wa Uimarishaji wa mfumo wa matukio ya kijamii uliofanyika katika Wilaya kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akipata maelezo ya kifundi kutoka kwa Mkurugenzi wa Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Matukio ya Kijamii Zanzibar Dkt. Hussein Khamis Shaaban mara baada ya uzinduzi wa Uimarishaji wa mfumo wa matukio ya kijamii na Jengo la Ofisi mpya ya Wilaya Dunga uliofanyika leo katika Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja, (kulia) Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dk. Ali Mohamed Shein, akihutubia wakati wa hafla hiyo ya Uzinduzi wa Ofisi za Wilaya za Usajili wa Vitambulisho vya Mzanzibar, katika viwanja vya Dunga Wilaya ya Kati Unguja.
WANANCHI wa Mkoa wa Kusini Unguja wakifuatilia hafla ya Uzinduzi wa Mfumo wa Usajili wa Kieletroniki na Ofisi za Usajili wa Vitambulisho Wilaya ya Dunga wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, akihutubia hafla hiyo.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, wakiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa SMZ na Wafanyakazi wa Wakala wa Usajili, baada ya hafla ya uzinduzi huo, uliofanyika Dunga Wilaya ya Kati Unguja
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.