Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambapo amesema kuwa wanawake hao kutoka vijiji tofauti waliingia ndani ya msitu kwa ajili ya shughuli mbalimbali zikiwemo kusenya kuni na kuchoma mkaa, ambapo walipatwa na mauti.
"Umbali wa kutoka kwenye vijiji vinavyozunguka msitu huo inakadiriwa kuwa wa Kilomita Tano hadi Sita, tuliwakuta wamepatwa na mauti, katika sehemu tofauti katika pori hilo, ambapo mmoja amekutwa amenyongwa huku dalili zikionesha alibakwa, alisema DCP Msangi.
Aidha Kamanda Msangi ameomba wananchi kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kwa lengo la kuwatambua watu wanaofanya matukio kama hayo, ambapo amesema kuwa amepeleka askari wa kutosha katika eneo hilo huku akiahidi kuwakamata watu wanaoendesha matukio kama hayo.
Pia Kamanda Msangi amewataka wananchi kutoingia katika msitu huo kama walivyotangaziwa na viongozi wao hapo awali na endapo wanataingia kwa ajili ya shughuli zao waingie wakiwa katika kundi ambapo amebainisha kuwa sehemu hiyo ni hatarishi na kuna wanyama kama nguruwe pori, fisi na viumbe wengine wanapatikana.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.