NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Kamanda mpya wa Jeshi la Polisi mkoani Mwanza ACP Jonathana Shanna, amezungumza na Maafisa wa Jeshi la Polisi mkoani hapa, ambapo ameonya kuhusu vitendo vya uhalifu na kuahidi kuvitokomeza kwa udi na uvumba.
Kamanda Shanna alifanya mazungumzo na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella baada ya kufika ofisini kwake kujitambulisha.
Naye Mongella alitumia fursa hiyo kuagana na aliyekuwa Kamanda wa Polisi mkoani Mwanza DCP Ahmed Msangi ambaye amehamishiwa Makao Makuu ya Jeshi hilo jijini Dar es salaam.
Aidha mazungumzo hayo yalijikita zaidi katika kuendelea kuimarisha hali ya ulinzi na usalama mkoani Mwanza, ambapo awali DCP Msangi aliwasihi maafisa hao kumpa ushirikiano wa kutosha kama waliokuwa wakimpa ili kutimiza vyema majukumu yake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.