NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Watanzania wameaswa kuwa na desturi ya kutembelea vivutio mbalimbali vya utalii nchini ili kuona na kujifunza mambo mbalimbali hususani mazingira, wanyama waliopo kwenye hifadhi zote na hata jiografia ya nchi.
Hayo yamesemwa na Afisa Habari wa Jiji la Mwanza Dkt. Elirehema Kaaya wakati akiwatembeza wageni kutoka Jiji la Wurzburg toka nchini Ujerumani waliofika Jijini Mwanza kutembelea na kufanya utalii kwa jiji hilo lenye urafiki na jiji walilotoka.
Wageni hao wameonekana kuvutiwa na majengo yaliyoachwa na ndugu zao zama za ukoloni sanjari na kustaajabishwa na maandhari nzuri ya miamba ya kuvutia katika jiji la Mwanza.
"Unaweza ukamuuliza mtanzania mwenzangu hii leo, Ni mbuga gani ya wanyama anayoifahamu akabaki kumangamanga asijue la kujibu, ile hali iko kilometa chache kutoka mji anao ishi lakini tizama ndugu zetu hawa wametoka maelfu na makumi ya maili na kilomita kwa nia tu ya kutembelea vivutio vyetu, hii ni aibu kwa wazawa wenzangu, tubadilike" alisema Dkt. Kaaya
UTALII WA NDANI NI NINI?
Utalii wa ndani ni
kule kutembea kutoka mahali pamoja hadi pengine ndani ya nchi husika. Tabia ya
watu kuthamini na kufanya utalii wa ndani inaweza kuchochewa kwa kuwapo sera za
utalii wa ndani kuanzia ngazi ya shule, vyuo, taasisi za dini na katika ofisi
mbalimbali za umma na binafsi.
Shule na vyuo zina
nafasi kubwa ya kuhamasisha kwa sababu zenyewe ni mojawapo ya wakala mkubwa wa
mabadiliko na maendeleo katika jamii. Kwa mfano, ni watu wangapi wanaofahamu
kuwa kuna aina rahisi ya utalii wa kufanywa kwa kutumia baiskeli?
CHUNGULIA KIDEO.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.