Shilole A.K.A Shishi Baby Kulia akiwa pamoja na Jackson Fute kuzindua rasmi riwaya waliyo andilka pamoja inayokwenda kwa jina la Broken Heart, uzinduzi huo ulifanywa ndani ya Duka la vitabu la Mak Books and Brains Mlimani City Jijini Dar es Salaam.
Kuhusu BROKEN HEART: Hakuamini mahusiano yake na mtu aliyempenda yaishe kwa yeye kudumbukizwa kwenye dimbwi la msongo wa mawazo, aliyempenda aligeuka kuwa adui.
'Mapenzi ni kitu ambacho kinaweza kukufanya chizi, sihitaji tena mwanaume maishani mwangu.' Alizungumza.
Lakini maisha ni safari, na akiwa katika safari ya maisha alijikuta akizama kimapenzi kwa mwanaume mwingine, mwanaume aliyedhani ni tofauti na waliopita.
Bwana Jackson Fute (Kushoto) akiongea na waandishi wa Habari Mara baada ya kuzindua riwaya waliyo andika na Shilole.
Msanii maarufu wa Muziki wa kizazi kipya Bongo Fleva, Bongo Movie na sasa Mtunzi wa vitabu Bi. Zena Yusuf Mohamed Maarufu kwa jina la Shishi Baby, akielezea kwa ufupi namna alivyopata wazo la kuandika Riwaya ya Broken Heart kuwa inalenga historia yake ya kweli kabisa na kuongeza kuwa amefurahi kumshirikisha mwandishi chipukizi Bw. Jackson Fute na kazi imeenda vizuri. pia aliwaomba watanzania wamuunge mkono kwani kitabu kinauzwa kwa Tsh 15,000 tu na Online Ebook ni Tsh 3,000 kinapatikana kote Duniani.
Mhariri wa Riwaya ya Broken Heart Bi Zuhura Seng'enge maarufu kwa jina la The African Lioness ambaye pia ni Mshairi, Mtunzi, Mwandishi na Mfasiri akielezea namna alivyo ipokea kazi ya kuhariri Riwaya hiyo na kukili kwamba ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufanya kazi hiyo. "Moja ya changamoto nilizozipata wakati nahariri Riwaya hii ilikuwa ni utamu wa simulizi zilizokuwemo ndani mpaka nikachelewa kumaliza kazi hiyo kwa muda kutokana na kunogewa na visa mkasa"
alisema Zuhura.
Waandishi wa Habari wakiendela kufanya mahojiano na Shishi Baby pamoja na Jackson Fute wakati wa uzinduzi wa Riwaya hiyo.
Mhariri wa Riwaya hii Bi. Zuhura Seng'enge akipokea Riwaya yake kutoka kw Shishi Bby
Mmoja wa wadau Bw. Hassan A.K.A Double D wa Uswahilini Matola nae akipokea Riwaya yake
Bw. David Kisamfu Akipokea Riwaya yake kutoka kwa Shishi Bby
Mtaalam wa picha za mnato Bw. Zajilu Zaid nae akionesha Riwaya yake ya Broken Heart baada ya kuinunua
Anaitwa Silver (kushoto) Akipokea Riwaya yake kutoka kwa Shishi Bby
Bw. Francis nae Akipokea Riwaya yake kutoka kwa Shishi Bby
Ukiingia tuu katika Duka la vitabu la Makbooks Brains Mlimani City utakutana na Riwaya ya Broken Heart
Mmoja wa wanunuzi akiwa anasoma Dibaji
Kulia ni mmoja wa wafanyakazi katika Duka la vitabu la Mak Books and BrainsBi. Fina akimpa mfuko wenye Riwaya ndani Shishi Baby ili amkabidhi mnunuzi.
Hili hapa ndio duka la vitabu la Mak Books and Brains lililopo Mlimani City hapa ndipo utapata Riwaya ya Broken Heart.
Picha zote na Fredy Njeje
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.