ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 29, 2018

PEMBE ZA NDOVU ZAWANG'OA KIBARUANI POLISI WAWILI MWANZANA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Askari Polisi wawili mkoani Mwanza wamefukuzwa kazi baada ya kubainika wakijihusisha na biashara haramu ya uuzaji wa nyara za serikali aina ya meno ya tembo kinyume na maadili ya jeshi.

Kamanda Shanna amewataja askari hao kuwa ni H. 5461 PC Enock na H. 4165 PC Robert ambao walikutwa na vipande viwili vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilogramu 20 katika eneo la Nyamhongolo Ilemela Mwanza.


"Kuna taarifa zilipatikana wapo watu wanaojihusisha na uuzaji wa meno ya tembo na Polisi walianza uchunguzi na kuwabaini Polisi hao waliokuwa wanashirikiana na watu wengine ambao na wao tunaendelea kuwasaka," alisema kamanda Shanna.

Kamanda Shanna amesema sheria ni msumeno na sheria ni kwa watu wote bila kujali tabaka hivyo amedai wanafanya msako kuwakamata wale wote wanaofanya kazi za magendo kwa kushirikiana na askari Polisi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.