ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 28, 2018

MTAWA AJIRUSHA KUTOKA GHOROFANI BUGANDO, AFARIKI DUNIA/AFANA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
MKURUGENZI wa Fedha na Mipango katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando (BMC) mkoani Mwanza Sr. Suzy Bathlomeo amefariki dunia baada ya kujirusha chini kutoka ghorofa ya pili.

Tukio la kujitosa kutoka ghorofa ya Pili limetokea Jumanne ya tarehe 27/08/2018 saa 11 alfajiri katika hospitali hiyo ya kanda ya ziwa baada ya kuwepo kwa tuhuma za upotevu wa fedha katika kitengo alichokuwa anakisimamia.

Na inaelezwa kuwa Mkurugenzi huyo siku chache zilizopita alikamatwa na Polisi jijini hapa kwa tuhuma hizo na kuhojiwa kisha kuachiwa kwa dhamana.

Aidha inadaiwa kuwa katika upotevu huo wa fedha kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni 300, watuhumiwa 9 walikamatwa akiwemo marehemu huyo ambapo wenzake wanane wapo nje kwa dhamana.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Kamishna msaidizi wa Polisi (ACP) Jonathan Shana akizungunza na waandishi wa habari hii leo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kamanda Shana amesema kuwa marehemu amefariki wakati akiendelea kupewa matibabu kufuatia kuumia vibaya katika maeneo ya kiunoni na mgongoni.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.