ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 28, 2018

MAKAMBA KUZINDUA MKUTANO WA KIMATAIFA WA MAZINGIRA.




Waziri we Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais January Makamba anatarajia kufungua mkutano mkubwa wa kimataifa unaohusu matumizi ya programu huria kwa usimamizi wa mazingira yaani FOSS4G 2018, jijini Dar es Salaam kesho.

Kwa mujibu wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira nchini (NEMC), Dk Vedast Makota mkutano huo muhimu unawakutanisha wataalamu kutoka pande zote za dunia kubadilishana uzoefu na kuhimiza matumizi ya teknolojia kuhifadhi mazingira.

“Mkutano huu unawaleta washiriki zaidi ya 600 ambao wamebobea katika masuala ya mazingira na matumizi bora ya teknolojia,” alisema Dk Makota na kuongeza kuwa mkutano huo una faida nyingi kwa Tanzania kama nchi.

Alisema mkutano huo unalenga pia kuhakikisha kuwa mataifa bila kujali uwezo wake yanakwenda sambamba na matumizi ya teknolojia kwa usimamivu endelevu wa mazingira.

Alisema mkutano huo mbali ya mambo mengine utasaidia kuimarisha uwezo wa Tanzania kama mwenyeji wa mkutano huo, kwenda sambamba na matumizi bora na endelevu ya mazingira kwa ustawi wa watu wake.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.