NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Naibu Waziri wa Kilimo Mhe.Dkt.Mary Mwanjelwa Agosti 04, 2018 amefungua rasmi maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nane Nane Kanda ya Ziwa Magharibi yanayofanyika katika uwanja wa Nyamhongolo Jijini Mwanza.
“…Maonesho haya ya Nane Nane ambayo ndiyo ya msingi sana, yasiwe tu kama ni maonesho ya nguvu ya soda, tunataka tuone matokeo chanya kwa wakulima wetu. Na kwa maana hiyo ifike mahala basi tuwe na maonesho ya kimataifa…”. Alisisitiza Dkt.Mwanjelwa.
Mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya maonesho hayo, Mathao Masele alisema yalianza Oktoba Mosi na yatafikia tamati Agosti 08, 2018 ambapo hadi sasa kuna zaidi ya washiriki 300 kutoka taasisi na makampuni mbalimbali.
Hii ni mara ya kwanza maonesho ya Kanda ya Ziwa Magharibi yanayoshirikisha mikoa ya Mwanza, Geita na Kagera kufanyika baada ya serikali kugawa mikoa ya Kanda ya Ziwa katika kanda mbili kwa ajili ya kushiriki maonesho ya Nane Nane. Kanda nyingine ni Kanda ya Ziwa Mashariki inayoshirikisha mikoa ya Mara, Simiyu na Shinyanga.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.