ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, July 6, 2018

SERIKALI YATANGAZA KIAMA KWA WABADHIRIFU VYAMA VYA USHIRIKA - DKT TIZEBA


Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 6 Julai 2018. 

Baadhi ya wananchi pichani wakimsikiliza Mgeni rasmi-Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akihutubia wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 6 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisisitiza jambo wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 6 Julai 2018.
Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba akisikiliza maelezo ya utunzaji fedha mara baada ya kutembelea banda la Mfuko wa kuendeleza sekta ya fedha Tanzania wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza, Leo 6 Julai 2018.

Na Mathias Canal-WK, Mwanza

Serikali imetangaza Kiama kwa viongozi na baadhi ya watendaji wa vyama vya ushirika waofanya ubadhilifu wa Mali za ushirika kwa manufaa yao pekee pasina kuwanufaisha wanachama wote.

Imeelezwa kuwa ubadhilifu wa rasilimali za ushirika unaofanywa na baadhi ya viongozi na watendaji wa vyama vya ushirika umekuwa ni tatizo sugu na hata kuwakatisha tamaa baadhi ya wananchi kujiunga na vyama hivyo.

Kalipio kwa wabadhilifu hao limetolewa na Waziri wa Kilimo Mhe. Dkt Charles Tizeba Leo 6 Julai 2018 wakati wa hafla ya ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la wanaushirika Tanzania linalofanyika katika uwanja wa Furahisha Jijini Mwanza.

Kongamano hilo la Siku mbili litaambatana na maonesho ya bidhaa na shughuli zinazofanywa na vyama hivyo vya ushirika kote nchini ambapo wanachama watapata fursa ya kubadilishana uzoefu, na kujadili mafanikio na changamoto wanazokabiliana nazo katika uendeshaji wa sekta ya ushirika nchini.

Dkt Tizeba aliwasisitiza washiriki wa kongamano hilo kutumia vizuri siku hizo mbili za kongamano hilo kwa ajili ya ustawi wa Maendeleo ya vyama vya ushirika na kujadili kwa kina namna bora ya uendeshaji na usimamizi wa vyama hivyo.

Alisema kuwa kauli mbiu ya siku ya ushirika Duniani kwa mwaka 2018 isemayo "Ushirika kwa ulaji na uzalishaji endelevu wa bidhaa na huduma" inakumbusha kwamba vyama vya ushirika sharti vihakikishe vinajitangaza na kutafuta Masoko ya bidhaa na huduma zake kwa jamii nzima.

Mhe Waziri wa Kilimo Dkt Charles Tizeba aliongeza kuwa serikali inatambua kuwa ushirika ni nyenzo muhimu ya kuwasaidia wananchi katika upatikanaji wa mtaji na kuwawezesha kuunganisha nguvu zao za kiuchumi katika kujiendeleza kiuchumi.

Alisema kuwa zipo juhudi kubwa zinazofanywa na serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wengi zaidi wanahamasishwa na hatimae kujiunga kwenye vyama vya ushirika kulingana na shughuli zao za kiuchumi ili kuondoa dhana kuwa vyama vya ushirika ni kwa ajili ya Kilimo cha Mazao ya biashara ya nchi za nje.

Sambamba na hayo Mhe Tizeba ameitaka Tume ya Maendeleo ya ushirika na shirikisho la vyama vya ushirika kuendelea kuwahamasisha wananchi kuendelea kutambua umuhimu wa kujiunga katika vyama vya ushirika kulingana na shughuli za wananchi mfano ushirika wa Viwanda, Madini, Ufugaji, Usafirishaji, Uvuvi na Kilimo.

Aliongeza kuwa serikali inatambua na kuthamini mchango wa ushirika wa Taifa katika kuyafikia malengo ya milenia na malengo mbalimbali ya nchi kama uimarishwaji wa sekta ya viwanda, Kilimo, uvuvi na biashara na kuchangia katika ongezeko la kipato kwa wananchi na hatimaye kuchangia katika ukuaji wa pato la Taifa 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.