NA ZEPHANIA MANDIA GSENGOtV
Baada
ya wanawake wanaouza miili yao maarufu kwa jina la "NZIGE"
kuvamia wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, Serikali imewataka wanaume wilayani
humo, kuachana na tabia mbovu ya kutumia fedha za mauzo ya mazao yao kwa matumizi ya anasa.
Kutokana
na uvamizi huo katika kata ya NUNDULU, kupitia Uzinduzi wa kampeni ya miezi
miwili, Serikali imewataka wanaume kutumia fedha kuendeleza familia kwa kujenga
nyumba bora na kusomesha watoto, waliotelekezwa bila malezi bora ya wazazi.
Juma Sweda ni Mkuu wa wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza, ameshiriki mstari wa mbele kuzindua kampeni maalum ya kutokomeza aina zote za ukatili wa kijinsia wilayani humo itakayodumu kwa kipindi cha miezi miwili.
Wilaya
ya MISUNGWI ni miongoni mwa maeneo ya mkoa wa MWANZA, ambayo wakazi wake licha
ya kuzalisha kwa wingi mazao ya chakula na biashara, lakini wameendelea kuishi
katika duni.
Maisha
hayo yanatokana na baadhi ya wanaume kutumia fedha za mauzo ya mazao kwa
matumizi ya anasa, na kusababisha wazazi wengi kushindwa kusomesha watoto na
kulalia magodoro yaliyotengenezwa kwa nyasi maarufu kama DODOMA NGUBALU.
Kwenye
uzinduzi huo, baadhi ya wanaume wamekiri kutumia fedha zinazotokana na mauzo ya
mazao kwa mambo ya anasa halmashauri
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.