ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, June 6, 2018

WATU 10 SASA WAFARIKI DUNIA BAADA YA AJALI YA GARI KUGONGA TRENI.KIGOMA.Taarifa zinasema idani ya watu waliofariki dunia sasa imefikia 10.
Watu hao mefariki dunia hapo hapo na wengine 28 kujeruhiwa, baadhi yao wakivunjika viungo kufuatia ajali ya basi la Ramida kugonga treni ya mizigo katika kivuko cha Gungu mjini Kigoma leo asubuhi.
Kwa mujibu Dr. Osimundi Diegula amesema kuwa majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Rufaa Maweni mkoani Kigoma ambapo ndiko idadi ilipoongezeka.

Ajali hiyo imetokea leo asubuhi, Juni 6 na imehusisha basi aina ya Tata Marcopolo lililokuwa linatoka Kigoma kwenda Nzega kupitia Tabora. Basi hilo lilikuwa na abiria 44.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, ACP Martin Ottieno amethibitisha kutokea ajali hiyo huku akitaja kuwa chanzo cha ajali ni uzembe wa dereva aliyeshindwa kuchukua tahadhari alipofika kwenye kivuko cha reli.
Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe ameandika katika ukurasa wake wa Twiiter akiomboleza vifo hivyo.
 Zitto amesema: “Nimezunguma na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) na tumekubaliana kuwa tuweke kizuizi katika eneo hili.”
Waziri wa Uchukuzi, Makame Mbarawa kupitia akaunti yake ya Twitter, ametoa pole kwa wakazi wa Kigoma na wananchi waliopoteza ndugu na jamaa kwenye ajali hiyo.
“Nitoe wito kwa watumiaji wa vyombo, ni vyema na busara kuwa waangalifu kwenye vivuko vyote vya reli,” amesema.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.