CHANZO/PARStODAY
Wabunge wawili wa eneo lenye mamlaka ya ndani la Hirshabelle nchini Somalia wameripotiwa kuuawa katika shambulizi la kuvizia la kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab, karibu na mji mkuu Mogadishu.
Meja Abdullahi Abdirahman, afisa wa Jeshi la Somalia ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa, wabunge hao waliuawa jana Jumanne baada ya gari lao dogo kushambuliwa kwa roketi na wanamgambo wa al-Shabaab katika kijiji cha Elka Gelow, yapata kilomita 45 kaskazini mwa Mogadishu.
Afisa huyo wa Jeshi la Somalia amewataja wabunge hao waliouawa kama Sheikh Dahir na Ismail Mumin na kuongeza kuwa, walinzi wao kadhaa pia waliuawa katika hujuma hiyo ya kigaidi.
Hata hivyo Abdiasis Abu Musab, msemaji wa kundi la al-Shabaab amesema waliteka nyaraka magari mawili, moja lililokuwa limebeba wabunge hao na jingine lililokuwa na walinzi wao wapatao 10, na kwamba wameua watu wote waliokuwa kwenye msafara huo.A
Haya yanajiri siku chache baada ya kundi hilo la ukufurishaji kuuteka mji wa Moqokori, ulioko yapata kilomita 300 kaskazini mwa mji mkuu Mogadishu katikati mwa Somalia, sambamba na kudai kuua wanajeshi 47 wa serikali katika makabiliano ya kuutwaa mji huo.
Tangu lilipofurushwa huko Mogadishu mwaka 2011, kundi hilo lenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa al Qaida limepoteza udhibiti wa miji na vitongoji vingi nchini Somalia.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.