ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, May 15, 2018

AHADI YA YANGA KWA MASHABIKI WAKE.

Kuelekea mchezo wa kesho wa Kombe la shirikisho Barani Afrika kati ya wawakikishi wa Tanzania Yanga dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda, Nahodha wa Yanga Nadir Haroub 'Cannavaro' amesema mchezo utakuwa mgumu kutokana na wapinzani wao kuwaheshimu kwasababu ni mabingwa wa Rwanda.

habari Jijini Dar es Salaam leo Mei 15, 2018 na kusema wanafahamu kuwa wapinzani wao ni timu nzuri ila nao wamejipanga vizuri katika mchezo huo.

"Tumejiandaa vizuri katika mchezo wa kesho japokuwa mchezo utakuwa mgumu kwasababu Rayon Sports ni timu nzuri na tunawaheshimu kutokana na kuwa ni mabingwa wa Rwanda. Hatuwezi kumdharau mpinzani, tunafahamu uzuri wao na ndiyo maana wamefika hapo walipo. Tumejiandaa vizuri lengo letu ni kushinda mchezo ili utuweke nafasi nzuri kwenye kundi", amesema Cannavaro.

Pamoja na hayo, Cannavaro ameendelea kwa kusema "wachezaji waliokuwa majeruhi wameshaanza kurejea na nadhani kikosi kitaendelea kuimalika kwa ajili ya mchezo huo".

Kwa upande mwingine, Cannavaro ameendelea kuwa sisitiza mashabiki wa soka hasa wanajangwani kujitokeza kwa wingi ili waweze kutoa sapoti kwa wachezaji ambao watakuwa wanacheza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.