Mbunge wa Chalinze, Mh. Ridhiwani Kikwete amefunguka na kuweka wazi kuwa klabu Yanga inahitaji mfumo sahihi wa uendeshaji wa mpira ambao utaweza kuwasaidia katika kukabiliana na changamoto mbalimbali hasa za kukosekana kwa pesa ili waweze kufanya vizuri katika michezo yao inayowakabiri.
Mhe. Ridhiwani ametoa kauli hiyo kupitia moja ya mijadala ambayo ilikuwa inaendeshwa katika mtandao wa kijamii twitter ukiwa na lengo la kutoa hamasa kwa mashabiki na wapenzi wa wanajangwani kujitokeza kwa wingi viwanjani ili waweze kujikusanyia mapato mengi yatakayotokana na watu kuingia uwanjani na sio kusubiri kuichangia muda ambao itakuwa imekwama kabisa.
"Yanga wanaitaji mfumo sahihi wa uendeshaji wa mpira utaolezea jinsi ya kukabiliana na changamoto ya kukosekana kwa pesa, kuacha kutegemea mtu, kutafuta vyanzo vya mapato vya uhakika, kulipa pesa kwa wakati na mengineyo yanayohusu mfumo wa mafanikio katika soka", ameandika Ridhiwani.
Licha ya Ridhiwani kutoa ushauri kwa Yanga lakini mmoja ya wadau waliokuwa wanachangia mjadala huo amesema "ukianza kuusaka huo mfumo bora wa kuindesha Yanga ndio wanatokea kina Akilimali wanaleta fujo, timu ikipoteza 'direction' nao wanakaaa kimya, 'so long as' kuna watu wana maslahi binafsi ndani ya Yanga, mabadiliko ni ngumu sana kuyapata".
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.