ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 7, 2018

USHER RAYMOND NA MKEWE WAACHANA.

It's over: Baada ya miaka miwili ya ndoa huku wakidumu takribani miongo miwili, Usher na mkewe Grace Miguel hatimaye wametangaza rasmi kuachana. (pictured November 2017) PICHA NA GETTY IMAGE.
Mwaka 2018 umeonekana kuwa ni mbaya kwa wapendanao. Usher Raymond na mkewe Grace Miguel wametangaza kuachana baada ya kupita miaka miwili ya ndoa yao na kudumu kwenye mahusiano kwa miaka 10.

Kwa mujibu wa mtandao wa Us Weekly umetoa taarifa ya wawili hao ya kuachana inayosomeka, “Baada ya kufikiria sana na kuzingatia tumeamua kujitenga kama wanandoa.”

“Tunaendelea kushirikiana kwa ukaribu zaidi, marafiki wa upendo ambao wataendelea kuunga mkono kwa njia nyingine ya maisha yetu. Kiasi kikubwa cha upendo na heshima tuliyo nayo kwa kila mmoja itaongezeka tu tunapoendelea,” imeongeza taarifa hiyo.

Hata hivyo Chanzo cha karibu cha wawili hao kimeuambia mtandao huo, Usher na Grace wametengana tangu miezi michache iliyopita.

Usher na Grace wamekuwa na mahusiano kwa karibu tangu mwkaa 2009 baada ya msanii huyo kuachana na aliyekuwa mke wake, Tameka Foster ambaye walifanikiwa kupata watoto wawili kwenye ndoa yao iliyodumu kwa miaka miwili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.