Wakati dunia iko katika wiki ya maadhimisho ya Siku ya Mwanamke, nazo Asasi mbalimbali za kiserikali na zile zisizokuwa za serikali zikiendelea na harakati zake kushiriki vyema katika hilo kwa nyanja na majukumu mbalimbali, Hospitali ya Rufaa ya Bugando ya jijini Mwanza nayo imekuja na hili la upimaji afya, utoaji elimu na tiba.
Kuanzia tarehe 8-9 (siku mbili mfululizo) Hospitali ya Rufaa ya BUGANDO kupitia madaktari wake wa ndani na mashirika nchi hisani, itatoa huduma ya upimaji afya ya FIGO bure kwa wanawake ikiwa ni pamoja na kuwapa elimu na tiba.
Alhamisi ya pili ya kila mwezi wa tatu ni Siku ya Figo Duniani nayo alhamisi ya tarehe 8 mwezi March mwaka huu 2018 imeangukia siku hiyo hiyo moja na Maadhimisho ya Siku ya Mwanamke Duniani.
KAULI MBIU YA MAADHIMISHO YA SIKU YA MWANAMKE KWA MWAKA 2018 INASEMA:- "Kuelekea uchumi wa viwanda tuimarishe usawa wa kijinsia na uwezeshaji wa wanawake vijijini"
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.