ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, March 7, 2018

HAJI MANARA AWAFUNGUKIA YANGA SC.


Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa klabu ya Simba amewaambia watani wao wa jadi Yanga SC kuwa aliwataka kuacha kuwazomea katika sare yao waliyopata juzi dhidi ya Stand United katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania Bara na badala yake wangetumia muda wao mwingi kujiandaa dhidi ya Township Rollers FC ya Botswana mchezo wa klabu bingwa Afrika.

Afisa huyo habari wa Simba SC ameyasema hayo kwa nyakati tofauti kupitia mtandao wake wa kijamii wa Instagram na radio.

Nyie Makida makida mlofungwa na Makiriri niliwaambia Juzi msijiandae kutozomea na kushangilia sare ya Stand. .nadhan sasa mtanielewa…kutwa mlikuwa mnahangaika na mechi yetu ya kesho….bumbaaav!!!!

Kupitia kipindi cha michezo cha E sports kinachoruka katika radio ya Efm Manara amesema kuwa Yanga wamepoteza kizembe kutokana na kutumia muda wao mwingi kuizungumzia mechi ya Simba tofauti na kujadili namna hipi watapambana na Township.

Manara ameyasema hayo baada ya mabingwa hao watetezi wa ligi kuu Yanga SC kukubali kipigo cha mabao 2 – 1 kutoka kwa wapinzani wao timu ya Township Rollers FC kutoka Botswana nchi ambayo linatoka kundi la muziki la Makirikiri.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.