Muheshimiwa Salaam,
Natumai u mzima wa afya.
Najua una nia nzuri ya kulinda maadili y amwafrika na hasa ya mtanzania na kuhakikisha basi hakuna ovu lolote linaloweza kuichafua sifa yetu lakini kubwa jamii zetu. Ila naomba nisahihishe approach yako.
Muheshimiwa kuna vitu vinaitwa Ratings nadhani huu ni Muda muafaka kwa tasnia yetu kuanza kua na hii system ili basi wasanii wafanye kazi kwa uhuru na pia hadhira (watazamaji na waskilizaji) pia wasipitwe ama kukosa kazi za wasanii wanaowapenda
Mfano wa ratings ni G ikiwa inamaanisha General yaani yeyote anaweza kutazama
PG hii inaweza tazamwa na yeyote ila watoto wanahitaji usimamizi wa wazazi kwani kuna baadhi ya material sio kwa ajili yao PG-13 wazazi wanahitajika, ikiwezekana aitazame movie, video yote kwanza kabla ya kumuonesha mtoto Na zingine kibao.
Hii ni 2018 sio mwaka 1903 sasa ivi tunachotakiwa kufanya ni kuanza kutambulisha hii system na sio kufungia nyimbo.
Lakini mbali na hayo, badala ya kushusha na kuzuia wasaniii kama kina @diamondplatnumz na wengine mlofungia kazi zao embu tazameni Tasnia nzima kwa ujumla.
Kuna watu wanatamani sana kuingia katika sanaa wakiwa na vipaji na uwezo ila wakiangalia yanayowakuta malegend kama kina majuto wanakata tamaa. Huwezi nambia mzee kama majuto leo na movie zote alizoekt hakuna kitu tasnia imeweza kumfanyia na yeye aishi kama hadhi ya jina lake.
Si majuto tuu wako wasanii wengi sana ambao wananafasi kubwa katika kuelimisha jamii lakini maisha wanayoishi ni tofauti na status zao. Je sanaa sasa ni kulinda maadili tu ama ni ajira pia?
Kazi za wasanii zinasimamiwa ipasavyo?
Je! Mnahakikisha kwamba wasanii hawanyonywi na mapromota?
Mnahakikisha kwamba hakuna watu ambao wao ndo wanajifanya Miungu wa kuwatawala wasanii na kuwanyonya wanaokataa kuwaabudu?
Ama wewe unaona kuzuia kazi ndo la msingi?
Unajua kwamba @diamondplatnumz ni msanii wa kimataifa kutoka Tanzania?
Unataka afate maadili ya kitanzania Jeh! Mashabiki zake wa nje nao kama wamarekani wanaishi maadili ya kitanzania? Kiti umepewa sio ulemaze sanaa yetu irudi nyuma, ivushe ifike mbali.
Badili sana yetu iwe accessible kimataifa sio kuiwekea mipaka.
Ni hayo tu Muheshimiwa naibu Waziri
Salaam kwako.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.