ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 11, 2018

ASKARI POLISI WILAYANI MAGU, WATAKIWA KUONGEZA JUHUDI YA KUKABILIANA NA UHALIFU.




 Na Mwandishi wa Polisi Mwanza: Oscar Msuya.

Uhalifu umepungua kwa kiasi kikubwa Wilayani Magu, hivyo askari ongezeni juhudi ya kukabiliana na uhalifu mdogomdogo unaoibuka katika baadhi ya maeneo. Hayo yamesemwa juzi tarehe 09/03/2018 na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, DCP: Ahmed Msangi wakati alipokutana na askari Polisi wa Wilaya hiyo wakati akiwa kwenye ukaguzi. Alisema anataka Magu iwe salama zaidi, kwani uwezo upo na hayo yatawezekana endapo wananchi watashirikishwa zadi. 
 Hata hivyo Kamanda Msangi amewataka askari Polisi kushirikiana na Idara ya Uhamiaji katika kukamata wahamiaji toka nchi jirani wanaoingia Wilayani hapo bila vibali. Alisema inasemekana wapo hivyo amewataka kushughulikia suala hilo mapema kabla hawajaleta madhara kwa wananchi.
Pia Kamanda Msangi amewapongeza askari polisi, vyombo vingine vya ulinzi na usalama na wananchi wa Wilayani hapo kwa ushirikiano mzuri uliopo wa kukomesha uhalifu hususani mauaji yatokanayo na imani za kishrikina. Amesisitiza ushirikiano huo usikome bali uongezwe haswa katika sehemu zenye uhalifu mdogomdogo “mfano wizi, ubakaji na migogoro ya ardhi” ili Magu iwe salama zaidi.

Kwa upande wa askari wa Kikosi cha Usalama barabarani amewasisitiza wafanye kazi kwa uweledi na haki, bila kumuonea mtu. Pia amewataka waepuke rushwa kwani ni kinyume na sheria, na kwa yeyote atakaye bainika hatua za kidhamu za kijeshi zitachukuliwa dhidi yake.

Vilevile amewasisitiza askari kuthamini kazi, ajira waliyonayo wailinde na kuithamini. Hivyo wajilinde wasije wakafanya mambo ya ajabu yatakayopelekea kufukuzwa kazi kwani Jeshi la Polisi linawapenda na kuwathamini.

Sambamba na hilo amewataka askari kuwa jasiri, wakakamavu, imara na uelewa mzuri wa mambo. Hivyo alisema anataka askari wafanye kazi kwa uweledi na wala sio vinginevyo. Pia amewataka askari wa upelelezi kufanya upelelezi kwa haraka na uweledi kisha mafanikio yapatikane kwa kesi wanazo zipeleleza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.