JANA Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA kupitia Kamati yake ya Maudhui iliketi na Wahariri na Wataarishaji wa vipindi vya Televisheni na Redio kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa, na kujadili masuala mbalimbali ya utendaji na utekelezaji pia kuzipitia kanuni ambazo ni msingi katika kulinda heshma ya Sekta ya Habari nchini, hii ni warsha iliyofanyika Jijini Mwanza.
Mada mbalimbali zimewasilishwa kwenye warsha hiyo ikiwemo Maudhui ya Kitamaduni iliyowasilishwa na Derrick Murusuri, Maudhui yanayolenga Maendeleo iliyowasilishwa na Joseph Mapunda pamoja na Misingi Bora ya Utangazaji iliyowasilishwa na Abdul Ngarawa.
Mada mbalimbali zimewasilishwa kwenye warsha hiyo ikiwemo Maudhui ya Kitamaduni iliyowasilishwa na Derrick Murusuri, Maudhui yanayolenga Maendeleo iliyowasilishwa na Joseph Mapunda pamoja na Misingi Bora ya Utangazaji iliyowasilishwa na Abdul Ngarawa.
Mada zote zimelenga kuwahimiza waandaaji wa vipindi kuzingatia sheria na kanuni za utangazaji na hivyo kuandaa vipindi bora vinavyochochea maendeleo ya taifa badala ya kuandaa vipindi vyenye mtazamo hasi katika jamii.
Lakini nao wadau wa Sekta ya Habari walikuwa na yao ya moyoni either yakushauri au ya kuwasilisha hoja ambayo waliyawasilisha na yakapatiwa majibu.
Kutoka kushoto ni Mkuu wa kitengo cha Habari ambaye pia ni Meneja msaidizi wa Radio jembe Fm, Harith Jaha akiwa na Mtayarishaji Mkuu wa Matangazo wa kituo hicho Oxy Okeleky (kulia) wakiwa katika warsha hiyo iliyoandaliwa na TCRA.
Sehemu ya wadau wa habari waliokusanyika hapa.
Wadau wa habari wakiwemo walaji (wasikilizaji) wamekutana hapa.
Viongozi wa Kamati ya Maudhui TCRA.
Uwasilishaji wa mada kwenye warsha hiyo.
Abdul Ngalawa akipita meza baada ya meza kwa washiriki katika kuwasilisha mada kwenye warsha hiyo.
Sehemu ya kusanyiko.
Wana Warsha.
Jiografia ya eneo la Warsha.
Kwa umakini wadau wakisikiliza huku somo wakilitafakari.
Majibu kwa kina toka kwa Joseph Mapunda.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.