Habari zilizotufikia muda huu ni kwamba leo January 2, 2018 wanamuziki Babu Seya na Papi Kocha wamekwenda kukutana na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.
Babu Seya na Papi Kocha walipokea msamaha wa Rais Magufuli kwenye Sherehe za Miaka 56 ya Uhuru December 9, 2017 na kuachiwa huru kutoka gereza la ukonga ambako walikuwa wakitumikia kifungo cha maisha tangu June 2004 baada ya kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti watoto.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.