ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 9, 2017

WAKIMBIZI WA KONGO DR WADAI KUWA JESHI LINAUA NA KUBAKA RAIA.

Wakimbizi wa Kongo DR wadai kuwa jeshi linaua na kubaka raia Maelfu ya wakimbizi raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo waliokimbilia nchi jirani ya Zambia wamelituhumu jeshi la nchi yao kuwa linahusika na mauaji na ubakaji dhidi yao.

Shirika la Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) limesema zaidi ya raia elfu sita wa Kongo DR wamekimbilia Zambia tangu mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu mpaka sasa, kupitia fukwe za Ziwa Mweru.

Kaimba Kazili, mmoja wa wakimbizi hao ambaye yuko katika kambi ya Nchelenge, kaskazini mwa Zambia ameliambia shirika la habari la AFP kuwa, wanajeshi wa serikali wanaua raia kiholela sambamba na kuwabaka wanawake kwa umati.

Mkimbizi mwingine kwa jina Mauno Rukogo ambaye amefanikiwa kuingia nchini Zambia akiwa pamoja na mumewe na wanawe wanne ameapa kutorudi DRC, akisisitiza kuwa ghasia zimeshtadi nchini humo na raia wasio na hatia wanauawa kiholela.

Wakimbizi wa Kongo nchini Zambia Haya yanaripotiwa chini ya wiki moja baada ya serikali ya Angola kuwafukuza nchini humo wahamiaji haramu wapatao 2,800 raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
 
Umoja wa Mataifa hivi karibuni ulitangaza kuwa, mapigano makali kati ya askari wa serikali ya Kongo DR na wanamgambo wa kundi moja la kikabila katika mkoa wa Kasai yamewalazimisha watu zaidi ya milioni moja kuyaacha makazi yao na kwenda kuomba hifadhi katika nchi jirani hasa Angola na Zambia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.