ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 29, 2017

MASAUNI, DK. MAKAKALA WAZUNGUMZA NA WAVUVI MKOANI MARA,WAWAASA KUSHIRIKIANA NA VYOMBO VYA ULINZI KUDHIBITI UHALIFU.



Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria, katika kijiji cha Nyang’ombe kilichopo wilayani Rorya, Mkoani Mara.Katika ziara hiyo Naibu Waziri aliambatana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala ikiwa na lengo la udhibiti uhalifu na uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala , akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria  katika kijiji cha Nyang’ombe kilichopo wilayani Rorya, mkoani Mara. Lengo la ziara hiyo ni   kudhibiti uhalifu na kudhibiti uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima, akizungumza na wananchi wanaoishi na kufanya shughuli zao za uvuvi Ziwa Victoria katika kijiji cha Nyangombe, kilichopo wilayani Rorya, mkoani Mara. Lengo la ziara hiyo ni  kudhibiti uhalifu na kudhibiti uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

 Mwananchi wa  kijiji cha Nyang’ombe akiuliza maswali kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni, wakati wa ziara ya kikazi ambapo naibu waziri aliongozana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dk. Anna Makakala, lengo la ziara hiyo ni kukagua  udhibiti uhalifu na  uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi

Wananchi wakishangilia jambo wakati Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani), akizungumza  katika mkutano uliofanyika kijiji cha Nyang’ombe ,wilayani Rorya. Naibu Waziri yupo katika ziara ya kikazi ikiwa na lengo la kukagua  udhibiti uhalifu na  uingiaji wa kinyume na sheria kwa raia kutoka nchi jirani.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO YA SERIKALI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.