Wakuu wa wilaya na
wakurugenzi wa halmashauri zinazolima zao la pamba mkoani Mwanza wametakiwa
kuacha mzaha na makapuni yanayoweka mkakati wa kutaka kuhujumu zao la pamba kwa
musimu 2017 /2018
Mkuu wa mkoa wa Mwanza
John Mongella amesema hayo katika kikao cha kuweka mkakati wa kilimo cha Pamba
mkoani Mwanza
Katika hatua nyingine mkuu
huyo amewaagiza wakuu hao wa wilaya kutoingia mikataba ambayo inaweza kudhofisha
kilimo cha pamba
Awali Mkuu wa idara ya
kilimo wilayani Magu Godleda Masale
akitoa taarifa ya maadalizi ya kilimo kwa musimu huu 2017 /2018 amesema kuna mkakati
wa kuongeza uzalisha kutoa kilo 300 kwa hekta moja mpaka 800 kwa msimu huu
Baadhi ya wakuu wa wilaya
zinazolima pamba mkoani mwanza wamesikitishwa na kitendo cha bodi kwa kusitisha
kilimo cha mkataba na baadhi ya makapuni ya kusambaza mbengu kushindwa kufikaia malengo
Kaimu Mkurugenzi wa Bodi
ya PambaTanzania Gabriel Mwalo amesema
kuwa bodi itahakikisha wakulima wote wanapata mbengu kwa wakati pamoja na
pembejeo hata wale ambao hawapo
kwenya kilimo cha mkataba.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.