|
Pichani
ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bwana FRANCIS Assenga akiwa kwenye
Kongamano la Biashara, Viwanda na Uwekezaji kati ya Tanzania na China
lililofanyika
katoka Hoteli ya Shangrila Jijini Guanzhou, China mwishoni mwa wiki,
ambapo pamoja na mambo mengine TADB iliweza kutangaza huduma zake na
jinsi fursa mbali mbali za kuvutia wawekezaji toka China na Ubia kwenye
miradi mbali mbali ya Kilimo nchini Tanzania ikiwemo
miundo mbinu ya Umwagiliaji; Maghala ya Kisasa na Masoko. |
Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeng'arisha Kongamano la
Biashara, Viwanda na Uwekezaji lililofanyika Jijini Guangzhou nchini
China mwishoni
mwa wiki; ambapo Viongozi wa Serikali, Sekta Binafsi na Wafanyabiashara
zaidi ya 80 toka Tanzania walihudhuria na kupata fursa ya kukutana na
kufanya mazungumzo ya uwekezaji na biashara na wenzao wa China.
Aidha, Benki ya Kilimo Tanzania iliweza kujadiliana na wadau mbali mbali wa kilimo kwenye mnyororo mzima wa thamani wa mazao ya
kilimo ambapo wengi walionesha nia ya kuja kuwekeza Tanzania.
|
Ujumbe
wa Tanzania wakiwa kwenye Picha ya Pamoja na Makamu Rais wa Mfuko wa
Maendeleo ya Africa wa China 'CADFUND". Kutoka kushoto ni Kaimu
Mkurugenzi wa Benki
ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) Bw. Francis Assenga, Katibu Mkuu
wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Bw. Adolf Nkenda, Makamu Rais na Naibu
Mtendaji Mkuu wa CADFUND, Bw. Wang Yong na Balozi wa Tanzania nchini
China Mhe. Mbelwa Kairuki, mara baada ya kumalizika
kwa kikao cha pamoja. |
Katika
Kongamano hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya
Killimo Tanzania Bw. Francis Assenga aliweza kuwa na mazungumzo ya kina
na Mkurugenzi
wa Shirika la Serikali ya China la Sinolight Holdings Corporation
linalojishughulisha na Uagizaji wa Mihogo toka nchi mbali mbali duniani
Bwana
Du Chuan ambako pamoja na masuala ya uwekezaji kwenye zao la
mihogo nchini, walijadiliana pia fursa zilizopo China kwa Watanzania
kwenye kilimo cha mihogo, hususan kwenye kuongeza thamani ya zao hilo.
|
Kaimu
Mkurugenzi Mtendaji wa TADB Bw. Francis Assenga kushoto akimkabidhi
zawadi ya Benki Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Maendeleo ua Afrika wa China
(CADFUND)
anayeshughulikia Viwanda, Kilimo, Afya na Uwekezaji Bwana
Lei Ma. Katikati ni Katibu Mkuu wa Viwanda Biashara na Uwekezaji
Prof. Adolf Mkenda na Kulia ni Makamu Rais na Naibu Mtendaji Mkuu wa
'CADFUND' Bwana Wang Yong mara baada ya kumalizika kwa Kikao baina yao
mjini Guangzhou juzi. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.