Airtel Timiza Vikoba suluhisho tosha vikundi vya akinamama
·
Kwa sasa ndio njia rahisi na nafuu kwa vikundi vya Vicoba kupata mikopo.
·
Kusambaa nchi kote hivi karibuni.
Huduma
ya Airtel Timiza vikoba imeendelea kuwa suluhisho tosha kwa makundi
ambayo yanataka kuweka akiba na kujipatia mikopo ili kuendesha biashara
zao vizuri.
Makundi
mengi ya Vikoba sasa hivi yameamua kutumia huduma ya Airtel Timiza
Vikoba kwani imewasaidia kuweka utaratibu mzuri huku serikali ikitaka
vikundi vya vikoba visambae zaidi nchini ili watu wengi waweze
kufaidika.
Hivi
karibuni akizindua mradi wa vikoba katika eneo la Bunju Jijini Dar es
Salaam, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi aliwataka viongozi
wa vikoba kuhaikisha wanatanua mitandao yao ili wananchi wengi zaidi
wafaidi.
“Natoa
wito kwa viongozi wa Vikoba kuhakikisha wanatanua mtandao wao wa vikoba
nchinzima ili watu wengi zaidi waweze kufaidi,” aisema Mkuu wa
Wilaya.
Airtel
Timiza Vikoba imekuwa gumzo kubwa sasa hivi hasa baada ya kampuni ya
Airtel kushirikiana na Benki ya Maendeleo kuhakikisha Vikoba vinakuwa
rasmi zaidi na vinafanya shughuli zake kwa umakini zaidi tofauti na
hapo mwanzo.
“Hadi
sasa tangu mradi huu uanze imeshatolewa mikopo 487 yenye thamani ya Tsh
milioni 20.5 kwa wanachama wa vikoba,” alisema Ibrahim Mwangalaba
ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo.
Alisema
jumla ya wateja 5,685 wameshajiunga na mfumo huu na kuunda makundi huku
akaunti mpya 1,1810 zikifunguliwa. Alitoa wito kwa wanachama
zaidi kujiunga na mfumo huo kwani ndio imekuwa suluhisho tosha kwa
matatizo yanayokumba vikundi vingi vya vikoba.
Tangu mradi huu uzinduliwe, makundi 18,166 yenye wanachama 178, 638 yameshasajiliwa Mwangalaba aliongeza.
Kwa
upande wake, Mkurugenzi wa Masoko na huduma ya Airtel Money wa Airtel
Tanzania Isack Nchunda alisema wanajivunia kwa kuweza kuleta suluhisho
na sasa hivi wamelenga kuhakikisha malengo ya serkali ya kuhakikisha
kunakuwepo na vikoba nchi nzima yanatimia kikamilifu.
“Makundi
mengi ya vikoba yalikuwa yanapata shida hasa katika kuweka kumbukumbu
na wakati mwingine vitabu vyao hupotea hivi kuwafanya washindwe
kuwa na kumbukumbu sahihi. Wengine walikuwa wanatunza fedha kwenye
vibubu, chini ya magodoro lakini huduma hii itawasaidia kuweka akiba zao
vizuri kupitia Airtel Money ambapo wanachama wote wanaweza kufuatilia,”
alisema huku akiongeza kuwa mwenyekiti tu ndiye
mwenye mamlaka ya kuwa na nywila wanachama wanatumiwa ripoti tu.
Alisema
huduma hii pia imesaidia kuimarisha uwazi katika makundi ya vikoba na
Airtel itaendelea kufungua milango zaidi ili kuhakikisha watu wengi
zaidi hasa wafanyabiashara wadogo wanapata huduma sahihi za kifedha.
Airtel Timiza Vikoba ilizinduliwa miezi mitano iliyopita ikiwa na lengo la kusaidia makundi mbalimbali kufikia malengo yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.