Naibu waziri mpya wa Wizara ya mifugo na uvuvi Abdallah Ulega
ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Mkuranga akifafanua jambo kwa waandishi wa
habari hawapo pichani mara baada ya kumaliza kikao cha kuzungumza na watendaji
wa Wilaya ya Mkuranga alipofanya ziara yake ya siku moja(PICHA NA VICTOR
MASANGU,)
Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya
Mkuranga Mshamu Munde akizungumza
ofisni kwake kuhusina na migogoro ya
ardhi iliyopo katika Wilaya hiyo,
Diwani wa kata ya Makamba Hassan Dunda akifafanua
jambo kuhusina na migogoro ya mshamba iliyopo katika halmashauri ya Wilaya ya
Mkuranga
(PICHA ZOE NA VICTOR MASANGU)
NA VICTCOR MASANGU, MKURANGA
NAIBU Waziri mpya wa
wizara ya Mifugo na Uvuvi Abdalah Ulega amesema hawezi kulifumbia macho hata
kidogo suala la baadhi ya viongozi na watendaji ambao wamekuwa na tabia ya
kufanya kazi kwa mazoea kwa kukaa tu ofisini bila ya kutimiza majukumu yao ipasavyo na kuwaagiza kuchapa kazi kwa bidii
bila ya kutegeana kwa kuvitembelea vikundi vyote vya uvuvi na ufuga ili
kuweza kusikiliza kero na kubaini changamoto zinazowakabili katika kutekeleza majukumu yao.
Ulega alitoa kauli
hiyo wakati alipofanya ziara yake ya kikazi ya siku moja kwa viongozi mbali mbali wa Halmashauri ya Wilaya ya
Mkuranga, ambapo amesema kuna baadhi ya
watumishi wengine wamekuwa ni wazembe na
kusababisha kukwamisha juhudi za serikali katika kuleta chachu ya maendeleo hivyo ameahidi kulivalia njuga suala hilo kwa
lengo la kuweza kuboresha sekta ya uvuvi na ufugaji.
Aidha Naibu Waziri huyo aliwataka maafisa uvuvi na mifugo kuwa wazalendo na nchi yao na kuhakikisha
wanazilinda na kuzitunza rasilimali
zilizopo pamoja na kuweka
mipango endelevu ya kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kufanyia kazi zao sambamba na kuviwezesha
vikundi hivyo katika mambo mbali mbali
ikiwemo kujenga,malambo, majosho pamoja na kuwapatia vitendea kazi.
Pia Ulega alisema kwamba kwa sasa
kipaumbele chake kikubwa ni
kuhakikisha kwamba anavisaidia kwa hali na mali kwa kuviwezesha vikundi
mbali mbali vya wafugaji na uvuvi pamoja na kuweka mipango madhubuti
ambayo
itaweza kusaidia kuleta mabadiliko chanya ya kimaendeleo katika sekta
hiyo
aliyopewa dhamana na Rais Dk. John Pombe Magufuli.
Naye Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga
Filbeto Sanga akizungumzia
kuhusiana na suala la ardhi alisema kuwa kumeibuka kikundi cha baadhi ya
madalali ambao ni matapeli wanachukua hela za
watu na kuamua kuuza maeneo ya mashamba ambayo tayari yana hati miliki
bila ya kufuata taratibu zozote na kupelekea wananchi wenyewe
kujikuta wanakosa maeneo kwa ajili ya kuendeshea shughuli zao za
kimaendeleo.
Katika hatua nyingine Mkugenzi
mtendaji wa halmashauri ya
Wilaya ya Mkurunga Mshamu Munde akizungumza katika kikao cha dharura na
waandishi wa habari ofisini kwake amekanusha uvumi wa taarifa
zinazotolewa na wananchi kuhusiana na shamba linalomilikiwa na
mwekezaji wa kampuni ya Soap Allied Industry .
Mkurugenzi huyo alifafanua kuwa eneo
hilo
ambalo linalalamikiwa na wananchi hao lina ukumbwa wa hekari 1750 na
kuongeza
kuwa kwa sasa linamilikiwa kihalali na mwekezaji huo tangu mwaka 1988,
na kupiga marufuku wananchi wanaovamia maeneo ya watu kiholela bila ya
kuzingatia taratibu.
“Mimi kwa kweli nina shangaa sana huu uvumi unaotokwa kwa baadhi ya wananchi
kuhusiana na eneo hili, ndugu zangu waandishi eneo hili linamilikiwa kihalali,
hivyo mimi ninachowaomba watu wanaolalamika kufika ofisi za mkurugenzi ili
niwape ufafanuzi zaidi na sio kuanza kusababisha migogoro ambayo haina faida hata kidogo katika Wilaya yetu ya Mkuranga nah
ii tabia kwa kweli mimi siwezi kuivumilia hata kigogo nitahakikisha kwamba
maeneo yote yanatolewa kwa utaratibu unaotakiwa,”alisema Mkurugenzi huyo.
Pia Mkurugenzi huyo alisema katikia kumuunga juhudi mkono Rais wa awamu ya
tano Dk. John Pombe Magufuli katika kuwa na Tanzania yenye uchumi wa viwanda
wameshatenga maeneo mbali mbali kwa ajili ya uwekezaji wa viwanda ambavyo
vitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa katika kukuza sekta ya viwanda na kuleta
maendeleo kwa wananchi pamoja na upatikanaji wa fursa za ajira kwa vijana.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri hiyo ya Mkuranga
Juma Abed na Diwani wa kata ya Makamba
Hssan Dunda hapa wanazungumzia kuhusiana na sakata hilo la mgogoro wa
shamba la mwekezaji huo na malalamiko
yanayotolewa na wananchi.
Walisema kuwa kwa sasa shamba hilo linamilikiwa kihalali na
mwekezaji huyo kwani alishakabidhiwa na halmashauri ya Wilaya ya Mkuranga baada
ya kufuata taratibu zote zinazostahili hivyo wananchi wanatakiwa kuachana na
tabia ya kuvamia maeneo mengine ambayo sio yao.
VITENDO vya uvamizi wa maeneo ya
mashamba pamoja na viwanja vinavyofanywa na baadhi ya viongozi wa na
wenyeviti wa vijiji kwa kushirikiana na
madalali ambao ni matapeli kwa kuvamia maeneo ambayo sio yao na kuamua
kuuza kinyemela kinyume na taratibu katika Wilaya ya
Mkuranga Mkoani Pwani vinachangia kwa kiasi kikubwa kutokea kwa migogoro
kila
kukicha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.