ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, October 12, 2017

BALOZI SIMBA AFUNGUA KIKAO CHA WADAU KUJADILI MABADILIKO YA SHERIA BARABARANI

Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Balozi Hassan Simba Yahya akizungumza wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Wadau wa Usalama Barabarani, kinachojadili mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa wizara, Joyce Momburi na Kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Japhet Lusingu.Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
 
Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Joyce Momburi, akizungumza na wadau mbalimbali wa Usalama Barabarani (hawapo pichani), wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Wadau wa Usalama Barabarani, kinachojadili mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani. Wengine ni Kamishna Msaidizi, Japhet Lusingu (kulia), Naibu Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Hassan Simba Yahya (watatu kulia) na Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Theopista Mallya. Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
 
Mdau wa Usalama Barabarani, Henry Bantu, akitoa Historia ya Baraza la Usalama Barabarani wakati Kikao cha Wadau wa Usalama Barabarani, kinachojadili mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani. Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
 
Mwanasheria wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Mrakibu Msaidizi wa Polisi, Deus Sokoni, akisoma vifungu vya Sheria ya Usalama Barabarani mbele ya wadau mbalimbali wa Usalama Barabarani (hawapo pichani), wakati wa Ufunguzi wa Kikao cha Wadau wa Usalama Barabarani, kinachojadili mabadiliko ya Sheria ya Usalama Barabarani. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Joyce Momburi na kushoto ni Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi, Theopista Mallya.Kikao hicho kinafanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay, Dar es Salaam.
 
IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA
MAMBO YA NDANI YA NCHI.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.